Facebook

Monday 25 May 2015

LIVERPOOL KUMTOA SADAKA LAMBERT ILI WAMNASE BENTEKE.

KLABU ya Liverpool iko tayari kumtoa Rickie Lambert ili waweze
kumsajili Christian Benteke kutoka Aston Villa.
Mshambuliaji huyo ni mmoja kati ya nyota waliopo katika mipango ya
usajili wa Liverpool majira haya ya kiangazi na wanaweza kuchuana
na Chelsea kuwania saini yake.
Hata hivyo Liverpool wanafahamu kuwa Villa walikuwa wakimtaka
Lambert Januari na wanaweza kuwa tayari kumuofa mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uingereza ili waweze kumpata Benteke.
Lambert mwenye umri wa miaka 33 aliamua kubakia Januari na
kupigania nafasi yake Anfield lakini Villa, Crystal Palace na
Bournemouth wote wameonyesha nia ya wazi kutaka kumsajilikiangazi
hiki.
Liverpool wamepania kufanya usajili mkubwa kiangazi hiki huku nyota
kama James Milner na danny Ings wote wakitegemewa kutua Anfield

0 comments:

Post a Comment