Facebook

Wednesday 20 May 2015

Yaya Toure njia nyeupe kujiunga Inter Milan.

Makamu wa rais wa Inter Milan ya Italia, Javier Zanetti amedai
kuwa klabu hiyo inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa
Manchester City Yaya Toure, 32.
Klabu hiyo ya Seria A, ambayo inafunzwa na maneja wa zamani wa
City, Roberto Mancini, inataka kumuondoa mchezaji huyo kutoka EPL
ambapo amekuwepo kwa miaka mitano.
"Tupo katika nafasi ambayo tuna matumaini ya kukamilisha," Zanetti
ameliambia gazeti la Italia la Gazetta dello Sport. "Yaya atatupa
ule ubora tunaouhitaji." amesema makamu wa rais wa Internazionale.

0 comments:

Post a Comment