Facebook

Thursday 28 May 2015

Nyuma ya Pazia kashfa iliyoikumba FIFA na Mr.Choi.

MR'GOLDEN-Oya haina kulemba ngoja tuone
nani ni sahihi maana kuna vitu huwa
unajifanya mbishi sana vingine sio vya kubisha.

MR'CHOI-Ah we jamaa bhana sasa unahisi wewe
utakuwa sahihi aya sasa mwaga
mchele mchangani tuuchambue alafu mwisho wa
siku tuone.

MR'GOLDEN-FIFA hili ni shirikisho la soka la
kimataifa Duniani ambalo
limekuwa likisimamia maswala yote ya
Kandanda Duniani likiwa limeanziswa
rasmi mwaka 1904 na Rais wa kwanza wa
shirikisho hilo alikuwa Mfaransa
Robert Guerin aliye dumu mpaka 1906 kisha
akamuachia Daniel Burley Woolfall
wa visiwa vya Malkia 1906-1918 kisha kina
Jules Rimet Ufaransa
1921-1954,Rodolphe Seeldrayers Ubelgiji
1954-1955,Arthur Drewry Uingereza
1955-1961,Sir Stanley Rous Uingereza tena
1961-1974,Dr João Havelange
Brazil 1974-1998 kisha akachukua madaraka
king'ang'anizi wa Uswisi Sepp
Blatter kwanzia 1998 mpaka sasa.

MR'CHOI- Sawa tunajua tuende kwenye lengo
lenyewe maana utanichosha na
hivyo vihistoria mwishoe nikose hamu ya
kujadili alafu tusogee chini ya mti
Jua lisha kuwa kali muda wa kufika Jahazi
bado.

MR'GOLDEN- Sepp Blatter amekuwa Rais wa
FIFA kuanzia mwaka 1998 ,katika
chaguzi zote 4 alizogombea Blatter amekuwa
akishinda huku kukiwa na mambo
mengi yakisemwa ikiwa ni pamoja na skendo za
rushwa safari hii Blatter yupo
tena kwenye Kinyang'anyiro cha kugombea urais
wa FIFA kwa mara ya 5.

MR'CHOI- Ndio yupo kama kawa utu uzima
dawa hizo skendo ni kawaida hakuna
sehemu isiyo na kasoro mbalimbali hata katika
familia yako kuna kasoro
kikubwa ni kuzipunguza maana hata kuzifuta
pana ugumu China yenyewe huwa
wananyonga ila jiulize bado watu wanapokea
rushwa .

MR'GOLDEN-Aaaa..wacha niseme,Blatter FIFA
pamemshinda,Nasema pamemshinda
huku tukihitaji kuona viongozi wapya wakiingia
madarakani ili kubadili au
kuboresha Kandanda ili uwe mchezo wa kisasa
zaidi Blatter ni kama Dikteta
anayetaka kuendelea kuiongoza FIFA kimabavu
ili hali FIFA pakiwa
pamemshinda.Narudia tena FIFA pamemshinda...

MR'CHOI- We rudia tena ikiwezekana tunga
kabisa wimbo ila hatoki mtu eti
dikteta kwa lipi sasa maana huwa uchaguzi
unafanyika na anashinda kihalali
ustake kuwaiga wa Libya ambao ''walifurahia
supu ya pelege wakajuzwa
kuongezewa supu ya pweza matokeo yake hivi
sasa hata hiyo ya pelege
hawaioni achilia mbali ya pweza wamebaki
kunywa supu ya dagaa.''

MR'GOLDEN-We jama bhana hivi unakumbuka
Mwaka 2014 wakati wa kombe la Dunia
Brazil ,MR.RAY WHELAN ambaye ni meneja
mkuu mtendaji wa kampuni ya mshiriki
wa FIFA,"Match Hospitality" alikamatwa ktk
hoteli moja huko Rio De Jeneiro
iliyokuwa ikitumiwa na maafisa wa shirikisho la
FIFA kwa kujihusisha na
vitendo vya uuzaji wa tiketi za kombe la Dunia
kinyume na Kanuni.Blatter
alichukua maamuzi gani ya maana katika hili?

MR'CHOI-......ah,ammmm eee aaah bhana e
hapo alikuwa bize na majukumu ila..?

MR'GOLDEN- Na bado ujashikwa na kigugumizi
Wacha nikukumbushe hili,Rais wa
UEFA Michael Platini wakati anajitoa kwenye
kinyang'anyiro cha urais wa
FIFA mwaka 2014 alisema,"Utawala wa Blatter
hauwezi kuwa mzuri kwa
maendeleo ya Soka" .Hii inaonesha ni jinsi gani
FIFA pamemshinda Blatter.

MR'CHOI-Kumbe alisema tu pasipo ushahidi
alafu kama kweli alikuwa
mpambanaji kwa nini alijitoa.? angepigana
mpaka mwisho tuone watu wengine
bhana.

MR'GOLDEN-Ushahidi upu kwani aliwahi kuitwa
kwenye kamati ya maadili ya
FIFA(2014) ili kuchunguzwa kuhusiana na
Kashfa za rushwa ,kwa maajabu na
kutokujitambua kwa Kamati ya maadili ilisema
Sepp Blatter alikuwa hana Kesi
ya kujibu na hapa ndipo tunapoona madudu ya
Rais Sepp Blatter na Kamati
yake.

MR'CHOI- Kweli kuna watu wana matatizo ya
ufikiri sasa kamati haikupata
makosa dhidi yake ulitaka iweje basi unda wewe
kamati au hao mnaomkashifu
mka mchunguze tena maana kuna watu
mnajifanya kuchonga tu kumbe ndo
walewale.

MR'GOLDEN-Sasa wacha nikurudishe nyuma
kidogo,Mwaka 2011 Makampuni makubwa
ya Coca Cola na Adidas ambayo ni wadhamini
wakubwa wa FIFA ,yalionesha
kusikitishwa na tuhuma za rushwa zinazotolewa
na FIFA ,Lakini Rais Sepp
Blatter alikanusha kashfa hizo bila kuzifanyia
uchunguzi wa kina.
Je,Tukisema FIFA pamemshinda
Blatter tunamkosea
heshima yake??

MR'CHOI-Hapaja mshinda na mnamkosea
heshima yake.

MR'GOLDEN-Aiseee......amini usiamini,Blatter
FIFA pamemshinda tena ni
wakupiga mawe anatuharibia soka tuhuma za
hongo ktk uenyeji wa kombe la
Dunia la Mwaka 2018 Urusi na 2022 nchini Qatar
ziliibuka ndani ya uongoz
huu- huu wa Blatter tena mpaka hongo za saa
zenye thamani ya Dola 25,000
kwa wajumbe wa kamati ya utendaji Choi
kwanini tusiseme Blatter ni Dikteta
asiyetaka kujiuzulu? we niaje..?

MR'CHOI- Tena hapo ndo usiguse kabisa hata
kama ila lazima apewe heshima
yake kwa kulieneza soka la kimataifa Duniani
kote na ndo maana
tukalishuhudia Asia 2002 likaja kwetu 2010 we
unadhani pasipo yeye ni lini
tunge shuhudia kombe la Dunia katika mabara
yote.? Acha ukuda wewe jamaa
sio mbinafsi na ndio kiongiozi bora anapaswa
kuwa kina Cameroon kimewachoma
kukosa nafasi na ndomaana wakaingiza bifu zao
za kisiasa na Urusi kutaka
asepe madarakani kisa wametoswa hivi wewe
hufikirii unadhani uwenyeji wa
kombe la Dunia angepewa Uingereza ungesikia
maneno ya kumkashifu...?

MR'GOLDEN- Ila kumbuka tuhuma zimeanza
kitambo tu usikurupuke Kama hiyo
haitoshi,mapema wiki hii Maafisa zaidi ya 14
wametuhumiwa kupokea rushwa
na kati ya hao tisa wapo madarakani sita
walikamatwa katika hoteli moja
mjini Zurich nchini,Switzerland. kwa tuhuma za
kujihusisha na vitendo vya
rushwa ya takriban kiasi cha dola za
Marekanimilioni 100 kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 20.

MR'CHOI-Dah unakurupuka vibaya kumbuka hao
maafisa walio kamatwa walikuwa
chini ya uongozi wa Mbrazil Dr João Havelange
1974-1998 maana wametenda
makosa kipindi cha mwaka 1990 wakati huo
Mzee wetu Blatter alikuwa katibu
mkuu 1981-1998 na kwa taarifa yako alikuwa
anajua swala hilo ndo maana haja
shangaa na anaunga mkono harakati zote za
kuwafagia wala rushwa na hii
imedhihirisha ni kiongozi bora kwa kutowakingia
kifua.

MR'GOLDEN- Ukweli ni kwamba Rais Sepp
Blatter hana sifa ya kuendelea kuwa
rais wa FIFA kutokana na Mlolongo wa Kashfa
za rushwa unaomkabili kwa
heshima ya soka ,Blatter anatakiwa kujiuzulu au
kuondolewa kwenye
kinyang'anyiro cha kugombea Urais ili kurudisha
hesima ya mchezo huu
unaopendwa na watu wengi Duniani mimi
hunielezi kitu wewe.
Alafu skia wewe dogo....
Wakati LUIS FIGO anatangaza nia ya kugombea
Urais wa FIFA
alisema,"Naangalia heshima ya FIFA kwasasa
siipendi,soka linastahili
uzuri.Katika wiki,miezi na hata miaka ya hivi
karibuni ,nimeona taswira ya
FIFA ikiporomoka.Baadae LUIS FIGO aliamua
kujitoa kwenye kinyang'anyiro
hicho baada ya kulalamikia mfumo wa
uendeshaji wa uchaguzi huo na kuuita
kuwa ni wakinafiki.
Naye rais wa chama cha soka huko
Uholanzi MICHAEL VAN PRAAG
aliamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais
wa FIFA baada ya kuona
mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi hauko sawa.

MR'CHOI- Oya mbona unaongea mfululizo naona
umepaniki dadeki utapiga deki
hapa alafu huyo alie jitoa hasahasa huyo Figob
bora alisepa maana
angeaibika mtu katoka kuwa balozi wa nyumba
kumi alafu anataka kuwa raisi
kwa misingi gani labda yani nampongeza
aliemshauri akajiudhuru , hao
wengine nao sikuona jipya kwao wasepe tu.

MR'GOLDEN-Hakika Blatter amejijengea ukuta
ambao ni vigumu sana kumuondoa
madarakani kwa njia ya uchaguzi huo ndo ukweli
na Kwasasa wamebaki wagombea
wawili,Sepp Blatter ambaye ni rais wa sasa wa
FIFA na PRINCE AL HUSSEIN
ambaye ni mwanachama wa kamati ya FIFA.
Tunahitaji kiongozi mpya atakayepambana
kwanza na hizi kashfa za rushwa
zinazoibuka kila kuitwapo leo kwenye shirikisho
la soka duniani FIFA ili
kuufanya mchezo wa soka uendelee kuwa na
ladha tunayoitaka wanasoka wengi
yote kwa yote Blatter hastahili kuendelea kuwa
rais wa FIFA.

MR'CHOI-Yamewashinda ya vyama vya soka
kwenye Wilaya zenu uje mpaka ngazi
ya Mkoa achilia mbali ya Taifa mtayaweza ya
Fifa wewe na hao pigeni
tarumbeta wee ila hata hapo mpaka wa Kenya
hayafiki wajua tatizo lenu
mmesha kopi tabia za waleee wanao waleteaga
misaada mwenye akili timamu
akichunguza atajua kuwa kosa la Blatter ni sera
zake za usawa kwenye mpira
Duniani kote.
Hata kama kuna tuhuma isiwe chanzo
cha mkashifu kwanza huyo
chambo PRINCE AL HUSSEIN amna kitu kabisaa
pigeni debe tu huyo Platin
alivyo mnafki anasukumia wenzake si ajitokeze
yeye.

MR'GOLDEN- Poa ngoja tuone ila ukweli
umejulikana Jahazi lile ubishi
uishe tuta tupana majini bure tusepe.

MR'CHOI-Poa ila najua wakati wa matokeo
utapita kushoto mimi kulia cha
msingi usinikimbie turudi wote huu mchele
ngoja ndege waje kula.

KWA MAONI;
Choikangta.ckt@gmail.com
titusdickson1@gmail.com

0 comments:

Post a Comment