Facebook

Sunday 24 May 2015

HAWA NDIO WACHEZAJI,MAKOCHA NA WAAMUZI AMBAO KUNA UWEZEKANO MKUBWA WAKAKOSEKANA MSIMU UJAO WA LIGI KUU NCHINI UINGEREZA

Si tu Raheem Sterling ambaye atatoa mkono wa
kwaheri kuelekea mechi za kufunga msimu leo hii wachezaji na makocha wa vilabu
mbalimbali watakuwa wakionekana kwa mara ya
mwisho kabisa katika vilabu vyao.
Didier Drogba anataraji kutoa mkono wa
kwahaeri kwa klabu ya Chelsea baada ya kurejea
klabuni hapa katika dirisha la majira ya joto
msimu uliopita. Ikumbukwe tu Drogba ni
miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na
misimu mizuri kabisa akiwa na klabu hiyo.

Makocha

John Carver (Newcastle United). Alikuwa ni
kocha wa muda wa klabu hiyo baada ya
kuondoka kwa Allan Pardew. Vipigo nane kati ya
michezo 10 ambayo klabu hiyo imecheza chini
yake ni ishara tosha kuwa kocha huyo hana
nafasi tena.

Sam Allardyce (West Ham United) Naye atatoa
mkono wa kwaheri klabuni hapo huku timu yake
ikiangalia kocha wa kumrithi.
Dick Advocaat (Sunderland) Bado ana hatihati ya kubaki hapo.

Wachezaji.

Danny Ings (Burnley) amefunga magoli 10 msimu
huu na anataraji kusaini katika klabu ya
Liverpool bure kabisa.

Didier Drogba (Chelsea) Anataraji kutoa mkono
wa kwaheri kwa klabu ya Chelsea baada ya
kurejea klabuni hapa katika dirisha la majira ya
joto msimu uliopita. Ikumbukwe tu Drogba ni
miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na
misimu mizuri kabisa akiwa na klabu hiyo.
James Milner (Manchester City) Naye ni kusuka
au kunyoa klabuni hapo.

Steven Gerrard anahitimisha kipindi cha miaka
17 ambacho ameitumikia Liverpool na kwenda
nchini Marekani kujiunga na LA Galaxy
Charlie Austin (QPR). Kama alivyo mwenzake
Ings, naye anatarajia kutimka QPR. QPR
watashudia pia Shaun Wright-Phillips, Rio
Ferdinand, Joey Barton, Richard Dunne, Bobby
Zamora, Karl Henry, Clint Hill na Alejandro
Faurlin wakiondoka pia.

David de Gea (Man Utd). Huyu yuko mbioni
kutimkia nchini Uhispania kujiunga na klabu ya
Real Madrid.

Brad Friedel anataraji kuondoka Tottenham
baada ya mchezo wa kesho, huyu atavunja
rekodi ya kuwa moja ya wachezaji wenye umri
mkubwa zaidi kustaafu soka akiwa na umri wa
miaka 44

Hugo Lloris (Tottenham). Huyu anaweza kwenda
Man United kurithi mikoba ya De Gea endapo
atatimkia Real Madrid.

Mario Balotelli naye ana hati hati ya kuondoka
klabuni Liverpool kutokana na kiwango duni
alichokionesha katika msimu mzima tangu
aliposajiliwa kutoka AC Milan.

Frank Lampard (Man City) huyu anatarajia
kuondoka Man City kwenda kujiunga na klabu ya
New York City.

Petr Cech (Chelsea). Hana raha katika klabu ya
Chelsea, yuko mbioni kutimkia ama klabu ya
Arsenal au Manchester United.

Kiungo wa Man City, Yaya Toure ana hati hati
ya kutimkia kunako klabu ya Inter Milan
kuungana na kocha wake wa zamani Roberto
Mancini.

Radamel Falcao atarudi katika klabu yake ya
Monaco baada ya kumaliza kipindi cha cha
mkopo katika klabu ya Man United, ambapo
hakuonyesha kiwango cha kuvutia mara baada
ya kufunga mabao 4, huku akiwa amewagharimu
Man United paundi milioni 24.

...Na mwisho ni Waamuzi.

Chris Foy anatarajiwa kustaafu baada ya
kutumikia kipindi chake cha uamuzi kwa miaka
14 akiwa ligi kuu nchini Uingereza pamoja na
michuano mbalimbali ya Ulaya.

Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment