Facebook

Saturday 30 May 2015

Sir Alex Ferguson amtabiria makubwa meneja wa Chelsea Jose Mourinho.


Kocha Jose Mourinho ametajwa wiki iliyopita kuwa kocha bora wa msimu wa Barclays.
Bosi huyo wa Chelsea hakuwepo kupokea tuzo yake usiku wa jana Jumanne.Lakini haikufanya Bosi wa zamani wa United kumpongeza.
Mourinho alihudhuria tuzo za mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea.
Sir Alex Ferguson anaamini Chelsea itapata mafanikio kwa kipindi kifupi
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United alimtangaza Mourinho kama mshindi.
Ingawa kocha huyo wa zamani wa Real Madrid hakuwepo, Lakini Ferguson alimzungumzia Mourinho kama mshindi na mafanikio yake kwa kipindi kifupi.


Fergie amesema 'Mourinho ni kocha aliyefanikiwa,aliyeshinda na anastahili hii zawadi, nafikiri alikuwa na kikosi bora na kapteni wake John Terry amecheza kila mchezo vizuri.
Mourinho ameiongoza timu yake kushinda kombe la nne la EPL ,ikimaliza na pointi 87 kushinda michezo 26, na kufungwa michezo mitatu, kutoka sare mechi 9, pamoja na kufunga magoli 73.
Akiongea kupitia rekodi ya video, Mourinho amesema 'nina furaha na fahari kupata tuzo hii, jioni yenye furaha kwenu na mapumziko mema, tukutane mwezi August.'amemaliza Mourinho.

0 comments:

Post a Comment