Facebook

Monday 25 May 2015

Said Ndemla amwaga wino Simba SC.

KIUNGO Said Hamisi Ndemla, amesema kwamba ataongeza juhudi ili kukuza kiwango chake na aweze kuisaidia timu yake, Simba SC kushinda mataji msimu ujao.

Akizungumza baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi leo, Ndemla amesema kwamba hiyo ni changamoto mpya kwake.“Kazi yangu nzuri katikamsimu huu imeishawishi klabu kunipa Mkataba mpya.

Hii ni changamoto kwangu, sasa naamini natakiwa kuongeza bidiiya mazoezi ili kukuza kiwango changu na kuisaidia timu yangu,”amesema.

Ameongeza; “Tuna kiu ya mataji, haswa taji la Ligi Kuu (ya Vodacom Tanzania Bara). Dhamira yetu kubwa msimu ujao tufanikishe azma hiyo.

Tunataka ubingwa wa Ligi Kuu,”amesema.Aidha, Ndemla zao la mradi wa soka ya vijana ya SImba SC, amewashukuru viongozi, wachezaji wenzake na benchi la Ufundi kwa ushirikiano wao kwake, ambao umemfanya leoawe mchezaji maarufu.

“Nawashukuru makocha wangu, haswa Matola (Suleiman) ambaye tulikuwa naye tangu Simba B.

lakini nawashukuru viongozi kwa kuniamini, na mimi nawaahidibaada ya kusaini, nitaongeza bidii niisaidie timu,”amesema.

0 comments:

Post a Comment