Facebook

Thursday 21 May 2015

Mwadui FC yamnasa mshambuliaji hatari,yamuongezea mkataba mnono Kocha Jamhuri Kihwelu.

Mbwembwe Dimbani's photo.
 MWADUI FC imefanikiwa kuinasa saini ya mfungaji hatari wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa2014/2015, Rashid Mandawa anaechezea Kagera Sugar.
Mandawa aliyefunga magoli 10 msimu wa ligi kuu uliomalizika mei 9 mwaka huu, leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia matajiri wa madini mkoani Shinyanga, Mwadui fc.
Wakati huo huo, kocha mkuu wa klabu hiyo ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Coastal Union, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ameongeza mkataba wa miaka mitatu (3) kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Julio pia alikuwa anawania na Wagosi wa Kaya baada ya kufaniikiwa kuwanusuru kushuka daraja.
Siku za karibuni, Mwadui ilimsajili Malegesi Mwanga kutoka Kagera Sugar, hivyo ni pigo lingine kubwa kwa ‘Wanankurukumbi’ wenye maskani yao uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.Kabla ya kujiunga na Mwadui, Mandawa alikuwa anaripotiwakuwindwa na Simba.

0 comments:

Post a Comment