Facebook

Thursday 21 May 2015

Juventus bingwa Coppa Italia

 
  Juventus wameibuka na ushindi mbele ya Lazio katika fainali ya Coppa Italia.
     Lazio ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Juventus mnamo dakika ya 4 kupitia kwa Radu baada ya kazi nzuri ya Cataldi.
     Hata hivyo bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 11 Chiellini aliisawazishia Juventus kwa pasi ya Patrick Evra
   Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa sare kipindi cha pili mchezo ulianza kwa kasi kwa pande zote kutafuta goli la ushindi lakini bado mambo yalikuwa magumu na mpaka dakika 90 zinamalizika bado kulikuwa hakuna mbabe.
   Mwamuzi wa mchezo huo
Orsato ikambidi aongeze dakika 30  ilikumpata bingwa
Alikuwa ni Matri mnamo dakika ya 97 alieingia kuchukua nafasi ya  Llorente akaipatia Juventus goli la pili na kuiwezesha timu yake kuchukua ubingwa wa pili msimu huu baada ya kuchukua ligi kuu hivyo macho yao ni kusaka ubingwa wa tatu kombe la mabingwa Ulaya mchezo utakao chezwa tarehe 6 /6/2015 dhidi ya Barcelona.

JUVENTUS WAMETWAA COPPA ITALIA MARA 10:
1937–38; 1941–42; 1958–59; 1959–60; 1964–65; 1978–79; 1982–83;1989–90;1994–95;
2014–15

0 comments:

Post a Comment