Facebook

Monday 25 May 2015

Arsenal yamaliza ligi kwa kishindo.

Mchezaji Theo Walcott amefunga mara tatu (hat-trick)na kuisaidia timu ya Arsenal kumaliza ligi kwa ushindi wa magoli 4 - 1 dhidi ya wageni West Brom.
1 - 0 Theo Walcott alitumbukiza mpira nyavuni dakika ya nne tu ya mchezo ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuanza toka mwezi March mwaka huu.
2 - 0 Walcott tena akawasurubu West Brom kwa goli la pili dakika ya 14.
3 - 0 Naye Jack Wilshere alifunga goli la tatu kwa upande wa Arsenal dakika ya 17.
4 - 0 Walcott tena akamaliza kazi kwa goli la dakika ya 37 ya mchezo huo.
4 - 1 Beki wa West Brom Gareth McAuley alifunga goli la kufutia machozi dakika ya 57.
Kocha Arsene Wenger anajiandaa kuiongoza timu yake katika fainali ya kombe la FA dhidi ya Aston Villa ili apate angalau kombe moja kwa msimu huu.
Timu ya Arsenal imemaliza kampeni ya ligi kuu ya Uingereza ikiwa nafasi ya tatu huku West Brom ikimaliza msimu nafasi ya 13.

0 comments:

Post a Comment