Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge
kwa siku kumi .
Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AFP
kuwa kufuatia jaribio la mapinduzi juma lililopita na vurugu
zilizofuatia ni bora kuahirisha uchaguzi huo kwa muda.
''Uchaguzi huo wa ubunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 26
mwezi Mei lakini sasa inatubidi kuihairisha ili kuwasikiza washirika
wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia
muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani.''
alisema Nyamitwe.
Hadi kufikia sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa
kufanywa Juni tarehe 26 haijabadilika.
''Subiri tu'' Nyamitwe aliwaambia waandishi wa habari.
Wanajeshi waaminifu kwa Nkurunziza walizima jaribio la mapinduzi
juma lililopita
Tayari rais Nkurunziza ametia sahihi amri hiyo ya kuhairishwa kwa uchaguzi.
Umoja wa mataifa ya bara Ulaya EU, na Umoja wa mataifa ya
Afrika AU, yametoa wito kwa uchaguzi huo uliokumbwa na utata
mkubwa uhairishwe ilikutoa fursa kwa mazungumzo ya upatanishi
kuendelea .
Hapo jana Rais wa Afrika Kusini alitilia pondo hoja hiyo ya kuahirisha
uchaguzi akisema ni bora uchaguzi huo uliopangwa ''uhairishwe''.
Takriban watu 20 wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na
waandamani katika mji mkuu wa Bujumbura kilele ikiwa ni juma
lililopita makamanda waasi walipotangaza jaribio la mapinduzi rais
Nkurunziza akiwa mjini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa
viongozi wa kanda uliolenga kutatua mzozo wa kisiasa nchini mwake.
Waandamanaji wamekuwa wakipinga kauli ya Nkurunziza ya kutaka
kuwania muhula wa tatu
Wapinzani wa rais Nkurunziza wanasema kuwa kutangazwa kwake nia
ya kuwania muhula wa tatu unakiuka sheria na makubaliano ya amani
ya mwaka wa 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe
vilivyodumu kwa miaka 13.
Nkurunzizakwa upande wake anashikilia kukutu kuwa ana haki ya
kuwania muhula mwengine kwani muhula wa kwanza hakuchaguliwa na
wanainchi bali wabunge.
Takriban watu laki moja wamekimbilia mataifa jirani wakihofia
kutibuka upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Wednesday, 20 May 2015
Rais Nkurunziza ahairisha uchaguzi Burundi.
Related Posts:
Rais wa Nigeria amekutana na wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram. Hatimaye Rais Goodluck akutana na wazazi Baadhi ya wazazi ambao watoto wao walitekwa nyara Rais wa … Read More
Wachunguzi waanza kazi Ukraine,kuhsiana na ndege iliyoanguka. Treni yenye mabaki ya waathiriwa wa mkasa wa ndege ya Malysia nchini Ukraine Makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo ilipoanguka ndege ya Malaysia … Read More
Shambulio katika kikosi cha Kumlinda Rais wa DRC lashundikana. Shambulio katika kambi ya jeshi ya kikosi cha kumlinda rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limezuiwa, kwa mujibu wa maafisa wa serikali. Hali imerejea kuwa ya utulivu na kundi dogo la "waliojipenyeza" limezid… Read More
Akaunti ya Twitter ya jeshi la Kenya yavamiwa Akaunti ya Twitter ya jeshi la Kenya pamoja na ile ya msemaji wa jeshi hilo imevamiwa na wanaharakati ambao wanaonekana kupinga ufisadi. "Nyote ambao mm… Read More
Wapalestina wengi wazidi kuawa Gaza Mmoja kati ya majeruhi wa mapigano eneo la Gaza Kumetokea vifo vingi katika eneo la Gaza kwa siku moja tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina mapema mwezi huu. Wapalestina zaidi ya sitini kati y… Read More
0 comments:
Post a Comment