Facebook

Monday, 1 June 2015

GUTIERREZ ATEMWA NEWCASTLE AMENDIKA UJUMBE MZITO;


Jonas Gutierrez ameibwatukia klabu yake ya Newcastle baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Muargentina huyo hatapewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Ilithibitishwa rasmi katika tovuti ya klabu hiyo kuwa Gutierrez, pamoja na Ryan Taylor, hawatapewa mikataba mipya na hivyo kuondoka klabuni hapo pindi mikataba yao itakapomalizaika Juni 30.
Gutierrez alirudi kundini mara baada ya kupona maradhi yake ya kansa ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu na kufanikiwa kupigania nafasi ya timu yake kubaki katika ligi kuu kwa msimu ujao.
Baada ya taarifa hizo za kuachwa na Newcastle kumfikia Gutirrez, aliandika hivi kwenye akaunti yake ya Twitter jana usiku:
'Two things I learn from my illness how you can support a player (newcastle fans) and how you leave a player alone (newcastle owner).
Akimaanisha kuwa:'Vitu viwili nimejifunza kutokana na maradhi yangu, cha kwanza ni namna gani ya kumsapoti mchezaji(hii ni kwa upande wa mashabiki wa Newcastle) na namna gani ya kumuacha mchezaji peke yake (hii ni kwa upande wa wamiliki wa Newcastle)'

Related Posts:

  • Mbeya City yafungua ukurasa wa usajili.Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Ndanda Fc, Gideon Benson amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu kujiunga na kikosi ch Mbeya City fc kinachonolewa na Juma Mwambusi katika msimu ujao Benson ameweka kando ofa kadhaa aliz… Read More
  • Chelsea yarusha ndoano kwa Gundogan.Timu ya chelsea inatajwa katika mbio za kuhitaji saini ya mchezaji IIkay Gundogan kutoka Dortmund lakini taarifa zinasema mchezaji huyo yupo katika mazungumzo na vilabu vingine vya Barcelona, Manchester United.Bayern na Ars… Read More
  • Man City yamnyatia Isco.Manchester City inataka kupata saini ya kiungo wa Real Madrid Isco. Mchezaji huyo miaka 23 hajui hatima yake Santiago Bernabeu baada ya ujio wa meneja mpya Rafa Benitez.Isco alijiunga na Real Madrid kwa ada ya Euro milioni30 … Read More
  • Tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo.Dau la Manchester United la pauni milioni 110 kwa Real Madrid kumtaka Gareth Bale, 25 na beki Rafael Varane, 22 limekataliwa na klabu hiyo ya La Liga (Daily Express),   Real Madrid wana uhakika wa kumsajili kwa pauni m… Read More
  • Singano "Messi" katika mtihani mzito Msimbazi. SIMBA SC inajipanga kumchukulia hatua mchezaji wake, Ramadhani Singano ‘Messi’ kwa kuituhumu klabu hiyo kughushi Mkataba wake. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara ‘Zungu’ amefanya Mkut… Read More

0 comments:

Post a Comment