Facebook

Friday, 14 November 2014

Equitorial Guinea kuandaa kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Taifa la Equitorial Guinea ndilo
litakaloandaa michuano ya dimba la
mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Kulingana na shirikisho la soka barani Afrika,
taifa hilo limetajwa baada ya Morrocco kukataa
kuandaa michezo hiyo kutokana na hofu ya
kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Morrocco ilikuwa imeiomba CAF kuahirisha
dimba hilo la January 17 hadi Feruary 8.
CAF vilevile imeipiga marufuku Morrocco
kushiriki katika dimba hilo ambalo sasa
litaandaliwa na taifa lililoandaa kombe hilo na
Gabon mwaka 2012.

Equitorial Guinea sasa itachukua jukumu lote la
kuandaa michuano hiyo yenye mataifa 16.
CAF imetangaza kuwa mechi hizo zitachezwa
katika miji minne ikiwemo Malabo,Mongomo
na Ebebiyin.Droo ya mechi hizo itafanyika
mjini Malabo tarahe 3 mwezi Disemba.
Haijabainika iwapo mwenyeji huyo mpya
atashiriki katika dimba hilo kwa kuwa timu
hiyo ilipigwa marufuku mwezi Julai kwa
kuchezesha mchezaji asiyetakikana katika
mechi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya
Mauritania mnamo mwezi May 17.

Related Posts:

  • John Bocco aanza mazoezi Captain John Bocco ameanza mazoezi kidogo kidogo katika Gym ya kisasa ya Azam FC hapa Chamazi - Azam Complex, Captain anaendelea vizuri na jeraha lake alilolipata Kigali Rwanda akiitumikia timu yake ya Azam FC. Hii ni leo asb… Read More
  • Jerry Muro apata ulaji Yanga SC.Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, ameondolewa kwenye nafasi hiyo na nafasi akapewa Jerry Muro mtangazaji wa zamani wa ITV na TBC1. Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa uamuzi huo wa Yanga ulitolewa katika kikao ki… Read More
  • Samir Nasri aziogopa Chelsea na Manchester United msimu huu.SAMIR Nasri anasema timu zitazotoa upinzani kwa Manchester City msimu huu ni Chelsea na Manchester United huku akisisitiza kwamba Liverpool watapata taabu kutokana na ushiriki wao wa mashindano mengi. - Una maoni gani juu ya … Read More
  • MZOZO WA NIGERIA NA FIFA WAISHAMabingwa wa Afrika, Nigeria huenda wameepuka kufungiwa kimataifa kuhusiana na mzozo wa uongozi katika chama cha soka cha nchi hiyo. Mzozo huo sasa umesuluhishwa, baada ya Chris Giwa kuondoa madai kuwa yeye ndio rais wa shirik… Read More
  • Danny Welbeck aing'arisha Uingereza.Danny Welbeck straika mpya wa Arsenal alifunga mara mbili kuisaidia England kuifunga Switzerland kwa bao 2-0 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2016. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United aliziona vyavu dakika ya… Read More

0 comments:

Post a Comment