Kamati za kudumu za bunge za mikopo za vyuo mbali mbali nchini mfano (DARUSO) zenye majukumu ya kufuatilia utekelezaji wa ahadi za serikali katika kutatua matatizo ya wanafunzi kwa mujibu wa kifungu cha 39(1) cha kanuni za bunge, zinaendelea kuwasisitiza wanavyuo wote mfano waUDSM waliokosa mikopo kukata rufaa(to appeal) bila kukata tamaa kwa utaratibu ufuatao:
*Unatakiwa kutumia M-pesa kama njia ya malipo kwa kuweka salio(5,000).
*Andika (*150*01#), kisha ponyeza kitufe cha kukubali(OK) na kisha fuata maelekezo.
*Ingia sehemu ya malipo, kisha malipo ya taasisi. Utachagua HESLB kisha utaweka kumbukumbu namba (reg. No. Form 4).
* Kiwango utaweka 5000 kisha password yako ya M-pesa.
*Mwisho utasubiri baada ya masaa kadhaa kwajili ya kupata receipt number. Utatembelea www.heslb.co.tz . User name utaweka namba yako ya usajili ya form4 na password utaweka receipt number utakayokuwa umepewa.
Ili kuongeza nafasi ya kupata mkopo, Kamati inashauri kuambatanisha vielelezo kama vyeti vya kifo, barua ya kustaafu kwa mzazi n.k
Pia inashauri kutochanganya taarifa ili kuondoa mashaka juu ya ukweli wa taarifa za maombi yako.
Kamati za mikopo ziko bega kwa bega na Umma wa wanafunzi wa vyuo nchini mfano UDSM.
Imeandaliwa na...........
Bob Chacha Wangwe
(M/kiti KAMATI-MIKOPO UDSM)
(M/kiti KAMATI-MIKOPO UDSM)
0 comments:
Post a Comment