Cristiano Ronaldo amekataa shutma kuwa
amemsema vibaya kinara mwenzie katika
kabumbu, Lionel Messi. kitabu kipya
kuhusu mshambuliaji huyo wa Barcelona,
kinaeleza kuwa mchezaji wa Real Madrid
mara kwa mara amekuwa akitumia maneno
ya kudhalilisha dhidi ya Messi.
Kumekuwa na tetesi kwa muda mrefu juu ya
kutoelewana kwa Ronaldo na Messi.
Ronaldo amesema kuwa hizi ni habari za uongo
na kusema kuwa atachukua hatua za kisheria
kuwashtaki wanaohusika na usambazaji wa
taarifa hizo.
Mchezaji huyo amejitetea kuwa anawaheshimu
wachezaji wenzie wote, akiwemo Messi.
Ronaldo amemaliza ubabe wa Messi wa kutwaa
tuzo ya Fifa ya mchezaji bora wa dunia kwa
miaka mitatu mfululizo, Ballon d'Or baada ya
kutwaa tuzo hiyo mwaka jana.
Zaidi ya yote wanandinga hao wametofautiana
kwa goli moja tu ili kuwa mfungaji bora wa
muda wote kwenye ligi ya mabingwa barani
Ulaya.Messi ana magoli 71 sawasawa na Raul
Gonzales wakati Ronaldo ana magoli 70.
Messi anahitaji magoli mawili tu ili kuwa
mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya
Hispania-La Liga,amefunga magoli 250 katika
michezo 285 nyuma ya Telmo Zarra wa
Athletic Bilbao aliyecheza miaka ya
1940-1950.
Thursday, 13 November 2014
Ronaldo akana 'kumponda' Messi
Related Posts:
TUZO ZA WACHEZAJI BORA WA MSIMU 2013/2014 - MAN UNITED > Tuzo ya Sir Matt Busby Mchezaji bora wa Mwaka - David de Gea > Mchezaji bora wa mwaka (aliyependekezwa na wachezaji wenzake) - David de Gea > Goli bora la msimu- Wayne Rooney vs West Ham United tarehe 22/03… Read More
Pep Guardiola alivyotia fora katika sherehe za Ubingwa Munich.... Pati la nguvu: Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola (kushoto) na mchezaji wake, Pierre-Emile Hojbjerg wakicheza dans jukwaani wakati wa sherehe za kufurahia kutwaa ubingwa wa Ujerumani, Bundesliga… Read More
Onyo kuhusu mkanyagano DRC Watu 15 wamefariki kufuatia mkanyagano uwanjani DRC Kumekuwa na shutuma kali dhidi ya mamlaka ya kandanda katika Jamuhuri ya kidemokrasia… Read More
KUELEKEA KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA - BRAZIL 2014 NIGERIA YATANGAZA KIKOSI CHAKE Makipa: Vincent Enyeama (Lille FC, France); Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheva, Israel), Daniel Akpeyi (Warri Wolves), Chigozie Agbim (Gombe United) Mabeki: Elderson Echiejile (AS Monaco, France); Efe Ambrose (Celtic, … Read More
Je timu ya mwisho duniani ni ipi ? Nicky Salapu ,kipa aliyeshiriki mechi waliofungwa 31-0 na Australia Mwaka wa 2001 timu ya Australia iliandikisha rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika kandanda ya… Read More
0 comments:
Post a Comment