
Tezi dume inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje (urethra).
Kwa kawaida tezi hii inauombo la wastani na huongezeka ukubwa kadri ya umri wa mtu unavyosogea.
Dk. George Mbaga kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anasema tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume.
“Kuna kifuko kiko kwenye kimrija cha mkojo kwa kiingereza tunakiita prostate gland, hicho kifuko kiko kwenye mrija wa mkojo,
mwanamume anapofanya mapenzi, manii yakitoka, kimfuko hicho kinatoa maji ya kuzirutubisha.

“Utafiti unaonesha ukifika miaka 50 kwenda juu, kile kimfuko kinakua kupita kiasi, mkojo unakuwa hautoki vizuri, unajisikia kweli haja ndogo lakini ukitaka kujisaidia mkojo hautoki au unatoka kidogo sana."
Dk. Mbaga alisema miongoni mwa vipimo ni pamoja na kile cha damu ambacho kitaalamu kinajulikana kama Prostate Specific Antigen (PSA).
Anasema kipimo hicho kinasaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH.
“PSA ni aina ya protini inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo mtu anatatizo na kufikia zaidi ya 500."
“Kipimo kingine ni Rectal Ultrasound, kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH."
“Ultrasound ya puru pamoja na kuonyesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH,”
anasema.
0 comments:
Post a Comment