Facebook

Wednesday, 5 November 2014

Wakazi waahidiwa dola mia kwa kukamata mbu Taiwan.

 Photo: DOLA MIA KWA KUKAMATA MBU
Wakazi katika mji mmoja nchini Taiwan wameahidiwa zawadi nono kwa kukamata mbu. Shindano hilo lilitangazwa na idara ya afya ya jiji la Kaohsiung, linalenga kupambana na mlipuko wa mbu wanaosababisha homa ya dengue katika eneo hilo. Wakazi wanatakiwa kukamata mbu wengi iwezekanavyo, wakiwa wazima au hata kama wamekufa, na mtu atakayekamata mbu wengi zaidi atapewa zawadi ya dola 100, imesema idara ya afya. Mshindi wa pili na wa tatu watapewa dawa ya kuzuia mbu na chandarua. Watu wanatakiwa kuwatega mbu hao, au kuhifadhi 'mizoga' yao, kwa sababu itawasilishwa mbele ya maafisa kwa ajili ya kuhesabiwa. "Badala ya kuwapiga faini watu wanaoshindwa kuweka mazingira safi, tunadhani mradi huu utasaidia kuhamasisha ushirikiano," amesema Ho Hui-ping, akizungumza na tovuti ya Focus Taiwan. Zaidi ya maambukizi 7,000 yameripotiwa mjini Kaohsuing, huku wagonjwa wapya mia mbili wakipatikana kila siku, limeripoti gazeti la China Post.

Wakazi katika mji mmoja nchini Taiwan wameahidiwa zawadi nono kwa kukamata mbu. Shindano hilo lilitangazwa na idara ya afya ya jiji la Kaohsiung, linalenga kupambana na mlipuko wa mbu wanaosababisha homa ya dengue katika eneo hilo. 
 
Wakazi wanatakiwa kukamata mbu wengi iwezekanavyo, wakiwa wazima au hata kama wamekufa, na mtu atakayekamata mbu wengi zaidi atapewa zawadi ya dola 100, imesema idara ya afya. Mshindi wa pili na wa tatu watapewa dawa ya kuzuia mbu na chandarua. Watu wanatakiwa kuwatega mbu hao, au kuhifadhi 'mizoga' yao, kwa sababu itawasilishwa mbele ya maafisa kwa ajili ya kuhesabiwa. 
 
"Badala ya kuwapiga faini watu wanaoshindwa kuweka mazingira safi, tunadhani mradi huu utasaidia kuhamasisha ushirikiano," amesema Ho Hui-ping, akizungumza na tovuti ya Focus Taiwan. Zaidi ya maambukizi 7,000 yameripotiwa mjini Kaohsuing, huku wagonjwa wapya mia mbili wakipatikana kila siku, limeripoti gazeti la China Post.

Related Posts:

  • Wafanyakazi waruhusiwa kuuchapa usingizi Kazini huko Korea Kusini. Serikali ya jiji, mjini Seoul, Korea Kusini, imeripotiwa kuruhusu wafanyakazi kulala mchana kazini ili kuongeza ufanisi, hasa katika miezi ya majira ya joto. Kuanzia Agosti 1, wafanyakazi wa serikali ya jiji la Seo… Read More
  • Ajira kwa watoto ruksa Bolivia.   Bolivia imeteremsha umri halali wa kufanya kazi ili kuruhusu watoto kufanya kazi kuanzia umri wa miaka 10 kwa masharti kuwa lazima waendelee kwenda shule na wawe wamejiajiri. Sheria hiyo pia inaruhusu watoto we… Read More
  • Libya yahofia kuporomoka Wanajeshi wa Libya wana wakati mgumu kukabiliana na makundi ya wapiganaji wa kiisilamu Libya imelionya baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba iwapo haitapata usaidizi wa kuimarisha vikosi vyake vya usalama ta… Read More
  • Watu 7 waua baada ya shambulio la Basi Lamu-Kenya    Watu wenye silaha wameua watu saba wakiwemo maafisa wanne wa polisi baada ya kushambulia basi la abiria katika kaunti ya Lamu kwenye mwambao wa Kenya. Watu hao walishambulia basi hilo kwa risasi karibu na… Read More
  • Rais wa Nigeria aomba msaada Serikali ya Nigeria inahitaji msaada wa dola billioni moja ili kukabilina na wanamgambo ambao wameliharibu taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni. Rais… Read More

0 comments:

Post a Comment