Facebook

Friday, 14 November 2014

Watoto watatu waongea lugha ya kipekee Uganda.

Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca
katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam
nchini Uganda wameanza kuzungumza
lugha tofauti isiojulikana baada ya
kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam
ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo
hilo.

Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia
ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
Kulingana ma gazeti la the monitor nchini
Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini
hawawezi kuzungumza na watu
wengine.Wanaamini tu kile baba yao
anachowaambia.

Kulingana na mama yao watoto hao waliweza
kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa
na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na
hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na
baba yao.

Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao
alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya
kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa
wadogo.

Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na
baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto
hao.

Related Posts:

  • Watu 50 wakamatwa wanaoshukiwa katika milipuko Kenya.   Naibu Rais wa Kenya Wiliam Ruto amesema washukiwa 50 wamekamatwa kuhusiana na machafuko yaliyotokea siku chache zilizopita katika eneo la pwani ya Kenya. Serikali imeahidi kuwasaka wote waliohusika na mashamb… Read More
  • Papa Francis aweka mambo hadharani Papa Francis jana alikukutana kwa faragha na kundi dogo la waathiriwa wa unyanyasaji wa kimapenzi waliotendewa na mapadri wa kikatoliki. Ni mara ya kwanza kukutana na waathiriwa hao tangu achaguliwe … Read More
  • AL Shabaab washambulia ikulu Somalia wapiganaji wa AL shabaab Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya hapo awali wapiganaji wa kiislamu kuishambulia. Maafisa wanasema washambuliaji wapa… Read More
  • Obama aomba msaada wa dharura Rais Obama ameielezea hali ya uhamiaji kuwa mzozo wa kibinaadamu Rais Obama anaomba dola bilioni 3.7 za msaada wa dharura kutoka bunge la Marekani kusaidia kukabiliana na ongezeko la watoto waliohama peke yao kutok… Read More
  • 20 wauawa katika shambulio la anga, Gaza Mashambulio ya anga yaliyofanywa na Israel yamewaua zaidi ya watu 20 katika eneo la Gaza, wakiwemo raia. mashambulio hayo yanatazamiwa kuwa mwanzo tu wa oparesheni kubwa inayopangwa kufanywa na Is… Read More

0 comments:

Post a Comment