
WhatsApp imewapunguzia sababu za kutojibu wale wote ambao huwa hawajibu ujumbe wa maneno {message} kwa wakatikwa kisingizio kuwa hawakuziona hata kama zilionyesha tiki mbili kuashiria zimefika.Hivi sasa WhatsApp wameamua kufanya mabadiliko katika mtandao huo baada ya kuongeza alama ya kuonyesha kuwa ujumbe umefika na muda uliofika ujumbe huo kama inavyoonyesha hapa chini
Kwa upande wa 'Group' tiki mbili za bluu zitakuwa zikionekana pindi tu watu wote kwenye 'group' wakiusoma ujumbe huo
Ili uweze kuona mabadiliko haya mtumiaji wa WhatsApp unashauriwa ku-Update 'Application' hiyo ya WhatsApp unayoitumia hivi sasa.
Mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii kwa hisia tofauti tofauti, wapo ambao hawajafurahishwa sijui wewe mdau wa Bantu upo katika kundi lipi?
Comment chini utupe mawazo yako katika hili.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kuongeza maarifa na kujua mambo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment