Indonesia imeshauriwa ikomeshe sheria inayowalazimu wanawake
kuthibitisha ni mabikira kabla ya kujiunga na jeshi la taifa.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameihimiza serikali ya
Indonesia kukomesha kipengee kimoja cha kubainisha iwapo
mwanamke ni bikira au la kabla ya kujiunga na jeshi la taifa.
Wanaharakati hao wanasema kuwa ni tukio linalodhalilisha wanawake
hao kwa misingi ya kijinsia.
Shirika la afya duniani WHO limepinga sheria hiyo likisema halina
misingi yeyote kiafya.
Aidha shirika la Human Rights Watch (HRW) inaongezea kusema
kwamba mtu kuwa au kutokuwa bikira hakuathiri utendakazi na
uwajibikaji wa mwanamke kazini.
Lakini je nini kinachoendelea Indonesia ?
Wanaharakati hao wanasema kuwa wengi wa makurutu ambao huwa
ni wasichana waliohitimu shule ya upili wenye umri kati ya miaka
18-20
hulazimika kukaguliwa sehemu zao za uzazi ilikuthibitisha wangali
''wasafi na hivyo wazalendo''
Kulingana na shirika la kutetea haki za kibinadamu, sasa hata
wachumba wa wanajeshi wao hawasazwi.
Indonesia yaombwa ikome kupima Ubikra
''wachumba wa wanamaji, wanajeshi wa angani na wanajeshi wa
ardhini sasa wanalazimika kupimwa ubikira kabla ya kuruhusiwa
kuolewa na maafisa''asema mwanaharakati mmoja.
Mwezi Februari maafisa wa jimbo la Jember ,Java Mashariki
waliharamisha kujaribiwa kwa wasichana kabla ya kuhitimu shule za
upili.
Je kipimo hicho kinafanywaje ?
Kulingana na mtafiti mmoja Andreas Harsono kipimo hicho
kijulikanacho kama "two-finger test", kinatumika na madaktari
kubaini iwapo mwanamke ni bikira au la.
Daktari anapaswa kung'amua iwapo mwanamke huyo ameshiriki tendo
la ndoa au la.
''Daktari anatumbukiza vidole viwili ndani ya uke na kimoja katika
tupu ya nyuma ''alisema mama mmoja mke wa mwanajeshi ambaye
pia ni askari.
Bwana Harsono aliwahoji wanawake 11 wengi wao wake wa wanajeshi
na wengine maafisa kivyao.
Hadi sasa haijabainika faida ya kipimo hicho ambacho kinalaumiwa
kuwa kinawadhalilisha wanawake.
Amiri mkuu wa jeshi la Indonesia Meja Jenerali Fuad Basya,amesema
kuwa kipimo hicho ni nguzo ya uzalendo na swala muhimu katika
usalama wa taifa.
''Haiwezekani iwapo mtu ni msherati si muaminifu kwa mumewe
apewe jukumu la kulinda usalama wa taifa''alisema Jenerali Fuad.
Kama mtu anapania kulinda mipaka ya taifa na pia usalama wa
mamilioni ya watu ilihali ameshasaliti nafsi ya mumewe basi mtu
kama huyo hapaswi kupewa jukumu la kulinda taifa''
Daktari akiandaa meza inayotumika kuwapima wanawake
''kama mwanamke si bikira iwe amegonjeka ama amejamiani hafai
kuwa askari Hafai kuhudumu katika jeshi la Indonesia '' Jenerali
Fuad alianukuliwa na vyombo vya habari.
Hata hivyo majibu yake yalitofautiana na ya mke mmoja wa
mwanajeshi ambaye mwenyewe ni askari aliyesema kuwa walipewa
sababu tofauti ya kipimo hicho.
''Wajua jeshi la Indonesia linataka wanajeshi wenye siha nzuri kwa
hivyo wanalazimika kutumia mbinu kama hizo kupunguza gharama za
matibabu ''
''Wanajeshi wetu wanasafiri kila baada ya muda na hivyo wanastahili
kuamini kuwa wanawake wao na hata waume pia ni waaminifu''
Monday, 18 May 2015
Indonesia yapigwa marufuku kupima 'bikra'
Related Posts:
208 wafariki kutokana na Ebola huko Guinea Maafisa wa afya wakiwazika waathiriwa wa homa ya Ebola Maafisa wa afya duniani wanaarifu kuwa watu wasiopungua 208 wameaga dunia kutokana na virusi vya Ebola nchini Guinea baada ya ugonjwa huo kusambaa kwa siku za … Read More
Baada ya tishio la Al Shabaab la kuua Viongozi Kenya,msafara wa rais ulinzi wahimarisha ni hatari..Jionee hapa Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kepkoitch anaripoti kwamba baada ya kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab cha Somalia kutoa onyo kwamba mashambulizi yake yanayofata yatawahusu viongozi wa Kenya, imebidi system ya … Read More
Pembe za ndovu zanaswa Mombasa Serikali ya Kenya imenasa shehena kubwa zaidi ya pembe za ndovu 228 katika kisiwa cha Mombasa mwaka huu. Shehena hiyo ya pembe za ndovu 114 ilipatikana katika bohari moja inayotumika na kampuni ya uchukuzi. Mshukiwa… Read More
DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23 Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeikashifu serikali ya Rwanda kwa kuwalinda wapiganaji wanaotuhumiwa kwa kusababisha mauaji ya halaiki chini ya nembo ya wapiganaji wa M23. Afisa mmoja wa Serikali ya D… Read More
Kuelekea Michuano ya Kombe la dunia,Polisi waongezwa mishahara Brazil Polisi waliandamana wakitaka nyongeza ya mishahara Serikali ya Brazil inapendekeza kuwapa nyongeza ya asilimia 15.8 mishahara polisi wake… Read More
0 comments:
Post a Comment