Facebook

Tuesday, 19 May 2015

Schneiderlin mbioni kuondoka Southampton kwa dau la Paundi Milioni 25.

KLABU ya Southampton inatarajia kutaka kitita cha paundi milioni
25 kwa ajili ya kiungo Morgan Schneiderlin mbaye anawindwa na
klabu za Arsenal na Tottenham Hotspurs.
Klabu hizo zinazotoka kaskazini mwa jiji la London, zote zimeonyesha
nia ya kumtaka kiungo huyo lakini Southampton wamedai
hawatamuachia chini ya kiwango hicho
. Southampton waligoma kupokea ofa yeyote kea ajili ya Schneiderlin
kiangazi mwaka jana, wakati mchezaji huyo alipojaribu kulazimisha
kuhamia Spurs.
Klabu hiyo imepania kufanya kama usajili wa kiangazi mwaka jana
ambapo walikunja kitita cha paundi milioni 25 kwa ajili ya Adam
Lallana na paundi milioni 20 kwa Dejan Lovren ambao wote
walikwenda Liverpool.
Arsenal wamepanga kutuma ofa ya paundi milioni 20 kea ajili ya
Schneiderlin wakati Spurs wao wako tayari kutoa kitita cha paundi
milioni 15.

Related Posts:

  • Walcott akataa kuzungumzia mkataba mpya ArsenalTheo Walcott hataki kuonyesha muelekeo wake ndani ya Arsenal ingawa mkataba wake umebakisha mwaka mmoja kuisha.Walcott alifunga katika fainali ya FA dhidi ya Aston Villa kwa ushindi wa 4 - 0.Mchezaji huyo ameviambia vyombo … Read More
  • Schneiderlin kutua Man United kwa ada ya Euro milioni 25Manchester United imevutiwa na kutaka kumsaini mchezaji kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin..Kiungo huyo wa miaka 25 ni mmoja wa viungo waliocheza vizuri msimu uliomalizika wa Premier League.Timu ya Arsenal na Tottenha… Read More
  • Yaya Toure 'Siondoki Man City'Mchezaji Yaya Toure amethibitisha kuendelea kukipiga Manchester City msimu ujao, na anafuraha na heshima kwake kuendelea kuwepo Etihad pamoja na kuwepo na uvumi wa kuhamia timu ya Inter Milan ya Italy.Kiungo huyo miaka 32 … Read More
  • Van Persie hatihati kusalia Man United Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie amekubali kuondolewa Old Trafford baada ya kupitia magumu msimu huu.Mshambuliaji wa Manchester United ana mwaka mmoja tu wa kumaliza mkataba wake wa sasa.Van Persie ana ma… Read More
  • Man United wapewa nafasi kubwa kumnasa Gundogan.Manchester United inamwinda mchezaji IIkay Gundogan kutoka Dortmund lakini taarifa zinasema mchezaji huyo yupo katika mazungumzo na vilabu vingine vya Bayern Munich na Barcelona. Timu za Arsenal, Chelsea zinatajwa kumchu… Read More

0 comments:

Post a Comment