Pata kujua kauli mbalimbali za viongozi wa kamati mbalimbali kwenye vikao vya Bunge la Kitiba Mpya vinavyoendelea hivi sasa Mjini Dodoma,viongozi hao wamewasilisha taarifa mbalimbali kutoka kwenye kamati zao,kama utaratibu ulivyopangwa;
Ni maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga
mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo
wa serikali tatu.
Tundu Lissu: ‘Nusu karne ya
uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na hakuwa na
mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania
kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi
hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji
kuelezwa ukweli’
Mchungaji Christopher Mtikila: ‘tulijengwa
kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi
yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano lilikua utapeli wa
kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari’
Mh Wassira: ‘Hati ya Muungano
ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa Mwenyekiti ndani ya
siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni kutaka kuvunja
muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta mgongano’
Mh Wassira: ‘Katiba ya Znz ndio
itabakia kuwa sheria kuu kwa Znz kwa mambo yasiyokua ya muungano,
tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata matatizo,
itapunguzia Wazanzibari fursa’
Ismail Jussa: ‘Hoja za historia
kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika mgando, ukiangalia
katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua Tanganyika na kuwepo
makamu wawili wa Rais’
Ismail Jussa: ‘Mkataba wa
muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo
ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokua Znz tunasema mengine tukija huku
tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu’
Ismail Jussa: ‘Zanzibar
tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa serikali
mbili Zanzibar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali kuendelea nao’
Ismail Jussa: ‘Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Znz kuondolewa kuwa makamu wa Rais’
Unaweza kuchangia mawazo yako hapo chini kama unalolote kuhusu kiako cha leo..............................endelea kupata taarifa na kutembele.............................................
http//www.katemimethsela.blogspot.com
Monday, 14 April 2014
UNAKIJUA WALICHOSEMA TUNDU LISSU, WASSIRA, JUSSA NA MTIKILA KATIKA KIKAO CHA BUNGE LA KITABA MPYA LEO?..Fuatilia Hapa.....
Related Posts:
Taarifa ya NCCR-MAGEUZI kwa Vyombo vya habari kuhusian na UKAWA.NCCR – MAGEUZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, DAR ES SALAAM, ALHAMISI, 17 SEPTEMBA 2015 USHIRIKI WA VYAMA VYA NCCR – MAGEUZI, NLD, CUF NA CHADEMA KATIKA UKAWA. UTANGULIZI Sisi viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha… Read More
BARUA YA BASHE NA SERUKAMBA KWA RAIS J.M KIKWETEBarua kwa Jakaya Kikwete Leo tunaomba tukuandikie barua Baba yetu Jakaya Mrisho Kikwete.......Kwanza kabisa pole sana na ugua pole.......Baba yetu Kikwete, tunaomba tukupe taarifa/ripoti katika kipindi hiki unapoendelea na ma… Read More
BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika magazeti yote ya leo Jumanne,Juni 2. MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu… Read More
Tazama picha za Mh.Benard Membe akiwa katika shughuli zake za kidiplomasia.Tazama picha za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Bernard Kamillius Membe akiwa katika kazi zake za kidiplomasia na viongozi wa kitaifa na kimataifa. … Read More
SIASA YA TANZANIA:-"RAFIKI WA MWIZI NAYE NI MWIZI" Maisha ya siasa hayana rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.Maisha ya kisiasa yamezungukwa na maslahi.Utashi binafsi na matamanio ya kiutawala… Read More
0 comments:
Post a Comment