Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la
Paulina (14) mwanafunzi wa darasa la tano
katika Shule ya Msingi Boko, jijini Dar
amekatisha masomo kutokana na kupata
ujauzito.
Mtoto anayejulikana kwa jina la Paulina
(14) alitundikwa mimba na mawanafunzi
mwenzake.
Akizungumza kwa huzuni huku akilia, mtoto
huyo alisema kwa sasa haendi shuleni
kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi
miwili alioupata kwa kijana aliyemtaja kwa
jina moja la Paulo mkazi wa Mbweni ambaye
ni mwanafunzi wa sekondari. Alisema
“Paulo alikuwa rafiki wa kaka yangu na
alikuwa akija sana nyumbani kwetu, tukawa
tumezoeana sana na siku moja akanishawishi
twende kwao, tukaenda na huko ndiyo
tukafanya mapenzi baada ya kuniambia
atanioa nikimaliza shule.
Mama mzazi wa Paulina, Luciana John
‘Mama Paulina’ (kushoto) akiwa na
mwanaye huyo.
“Alikuwa akinipa fedha mara nyingine elfu
mbili au tatu ambazo nilikuwa nikizitumia
shuleni, mwishowe ndiyo nikanasa,” alisema
Paulina.
Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto
huyo ambaye kazi yake ni kugonga mawe
maeneo ya Chasimba, Boko, Luciana John
‘Mama Paulina’ alisema anaumia sana kwani
alikuwa akitegemea mwanaye asome ili aje
kumtoa kwenye shida lakini badala yake
amepata mimba tena ya utotoni.
Imeelezwa kuwa, tukio hilo limefikishwa
kwenye vyombo vya sheria ili binti huyo
aweze kusaidiwa.
Saturday, 1 November 2014
MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO ATUNDIKWA MIMBA NA MWANAFUNZI MWENZAKE KISA SH.ELFU MBILI
Related Posts:
Serikali yalifungia gazeti la 'Mawio'.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni… Read More
Rais Dkt. J.P Magufuli 'atumbua majipu' Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa.Rais Magufuli ameamuru kurudi nyumbani mabalozi sita haraka akiwemo Dr Batilda Buriani, Dr James Nsekela wa Italia na Peter Kalaghe wa Uingereza Pia Mkurugenzi mkuu wa NIDA Bw Mwaimu amesimamishwa kazi kuanzia sasa. Akitangaz… Read More
TAKUKURU: Kesi ya Ukwepaji Kodi ya LAKE OIL mtuhumiwa amepewa miezi miwili kurejesha Kwa umma Bilioni 8.5! TAKUKURU: Kesi ya Ukwepaji Kodi ya LAKE OIL mtuhumiwa amepewa miezi miwili kurejesha Kwa umma Bilioni 8.5! … Read More
Taarifa kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa kuhusiana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha Nchini. … Read More
Serikali yatoa ratiba mkutano wa Wazalishaji Umeme Wazalendo.WAZALISHAJI UMEME WAZALENDO Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM, Jumatatu, 18-1-2016: WIZARA ya Nishati na Madini imeandaa mkutano wa wazalishaji umeme wazalendo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar. "Wizara itatoa ratiba kwa… Read More
0 comments:
Post a Comment