Facebook

Monday, 14 April 2014

CHELSEA YAKOMAA NAFASI YA PILI


Chelsea ilisalia katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza licha ya kuilaza Swansea bao moja kwa bila katika mechi ngumu iliyochezwa jumapili .
Mlinzi wa Swansea Chico Flores alionyeshwa kadi za njano mbili na akalazimika kuondoka uwanjani katika dakika 16 tu ya kipindi cha kwanza .
Vijana wa Jose Mourinho walilazimika kufanya kazi ya ziada.Na kufanikiwakupata bao lao la pekee lililofungwa na Demba Ba kunako dakika ya 68 ya kipindi cha pili .
Ba itakumbukwa aliisaidia Chelsea kuilaza Paris-St Germain katika mechi ya kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya jumanne iliyopita.

Ratiba ya Chelsea Michezo iliyobaki

19 April: Sunderland (H)
22 April: Atletico Madrid (A)
27 April: Liverpool (A)
30 April: Atletico Madrid (H)
4 May: Norwich (H)
11 May: Cardiff (A) 

Kutokana na kichapo hicho,Swansea imeporomoka hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 20.
Kwa upande wa Chelsea wamesalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 75 alama mbili nyuma ya vinara Liverpool waliosajili ushindi mkubwa wa mabao 3-2 dhidi ya wapinzani wao wakuu Manchester City katika mechi
iliyochezwa mapema jumapili.
Manchester city sasa iko katika nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya alama 70 lakini ikiwa na mechi mbili zaidi za kucheza.
Liverpool imesalia na mechi nne pekee.
Everton imeipiku Arsenal Katika nafasi ya nne ikiwa na alama 66 mbili zaidi ya The Gunners ambao sasa wanajikita katika nafasi ya 5.
Tottenham ni ya sita na alama 60 huku Manchester United wakiwa katika nafasi ya 7 na alama 57.

0 comments:

Post a Comment