Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema
kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari
lake aina ya Volkswagen.
Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini
duniani kutokana na maisha yake ,alisema
kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja
wa dini ya kiislamu katika eneo la uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda
kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha
hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe
anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake
kwa watu masikini.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa
inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari
lake la Volkswagen
Busqueda liliripoti kwamba ombi la gari hilo
lilifanywa katika mkutano wa kimataifa
mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz
Bolivia.
''Nilishangaa mara ya kwanza ,a hivyobasi
nikapuzilia mbali.lakini baadaye ombi jengine
lilikuja na hivyobasi nikaanza kulichukulia
kuwa swala la umuhimu'',. Alisema Mujika.
Saturday, 8 November 2014
Rais masikini zaidi duniani apewa dola milioni 1
Related Posts:
Uganda yasema haitishwi na vikwazo Gazeti la Red Cross lilichapisha majina ya watu wanaoshukiwa kuwa wapenzi wa jinsia moja baada ya sheria kupitishwa Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa… Read More
Wanaharakati 8 washtakiwa Mombasa, Kenya Mombasa ni moja ya miji ambayo imeshuhudia utovu mkubwa wa usalama Wanaharakati wanane wamefunguliwa mashitaka mjini Mombasa Pwani ya Keny… Read More
Ndege zisizo na rubani kutumiwa Mali Hali nchini Mali bado ni tete kwani usalama bado haujapatikana tangi vita kuanza Ndege zisizo na rubani zitaanza kutumiwa na Umoja wa Mat… Read More
Rais wa Malawi kumuoa mpenzi wake Rais Mutharika (kulia) ana umri wa miaka 74 Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika anatarajiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu,mwishoni … Read More
Onyo kwa wakenya kuhusu kombe la dunia Shambulizi la hivi karibuni kukumba Kenya ni la Mpeketoni ambapo watu zaidi ya sitini waliuawa Serikali ya Kenya imewataka raiya kuwa waangalifu na kuwa… Read More
0 comments:
Post a Comment