Facebook

Monday, 10 November 2014

wanafunzi 23 wauawa shuleni Nigeria.

 
Kumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Hata hivyo hakuna taarifa kamili kuhusu idadi ya majeruhi kufikia sasa ingawa duru zinasema kuwa wanafunzi kadhaa wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Shambulizi lilitokea wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji wa Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.
Shule hiyo ni ya mafunzo ya sayansi. Mwalimu mmoja alinukuliwa akisema kuwa alisikia mlio mkubwa wa kutisha wakati bomu hilo lilipolipuka.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram huenda ndilo limefanya shambulizi hilo, ila taarifa bado hazijathibitisha hilo.
Kadhalika kundi hilo limekuwa likishambulia shule katika harakati zake za miaka 5 likitaka kuunda dola ya kiisilamu huku likipinga elimu ya kimagharibi.
Wiki jana shambulizi la kujitoa mhanga lilifanyika mjini humo na kuwaua watu 15 wakati wa maandamano ya kidini.

Related Posts:

  • KESI YA KENYATTA YAPIGWA KALENDAWaendesha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC iliyopo The Hague wameomba kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuahirishwa tena. Bwana Kenyatta anashtakiwa kwa makosa dhidi ya ubinaadam, lakini upande wa mashtaka umes… Read More
  • Watu 200 wauawa na mafuriko huko Kashmir Mafuriko yamewaua zaidi ya watu 200 nchini India na Pakistan huku watabiri wa hali ya hewa wakisema kuwa mvua zaidi inatarajiwa kunyesha. Majeshi ya ma… Read More
  • Damu ya waliopona Ebola kutibu Wagojnwa wengine. Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wamepona ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwatibu wagonjwa wengine. Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya… Read More
  • HATIMAYE KIONGOZI WA AL SHABAB AUAWA Aliyekua kiongozi mkuu wa Alshabab Ahmed Abdi Godane ameripotiwa kuuawa!! Habari kutoka katika idara kuu ya ulinzi ya marekani PENTAGONI imesema kua kuuawa kwa kiongozi huyo mwanzilishi wa kikundi ambacho kimekua mwiba mkali… Read More
  • Alshabaab wathibitisha kifo cha kiongozi wao,Godane Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani. … Read More

0 comments:

Post a Comment