
Wanaharakati wa haki za binadamu
wanalishutumu Jeshi la Iraq kwa kushindwa kuokoa maelfu ya watu kufikia
sehemu salama ya nchi hiyo mara baada ya wao kukimbia mapigano katika
jimbo la Anbar .
Wanaharakati hao wanasema serikali - ambayo
inawaongoza ina waslamu wengi wa madhehebu ya Shia inawabagua Waisalamu
wa madhehebu ya Suni waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya
Islamic State aambao nao pia ni Waislamu wa Suni.
Kwa wale
wanaojaribu kuingia Baghdad wanakutana na vikazo vya barabarani katika
mitaa ya mji ambapo hatua za kiusalama kwa ajili ya ulinzi
zinachukuliwa.
Familia za Sunni zimekutwa zikiwa
zimekwama eneo hilo zikiwa na hali mbaya ambapo wanafikiria kurejea
kwenye maeneo yaliyoshikiliwa na IS.
0 comments:
Post a Comment