Mimi nasema tena kuwa mimi nimwanachama hai wa CHADEMA, Nimemsema mh.
Mbowe kwakuwa yeye ndiye mwenyekiti wetu na mkuu wa kambi rasmi ya
upinzani bungeni, haya yanayoendelea kukishushia heshma chama hayaoni?
Dr. Slaa naye kama katibu wa chama hayaoni?.
Ni aibu kubwa sana taasisi kubwa kama hii yenye watu makini kiasi hiki
kupambana na mtu mmoja tena mwisho wake tunaishia kupata aibu.
Kwani faida yetu sisi wananchi na wanachama mkimmaliza Zitto Kabwe kisiasa ni ipi?
Hapo awali mmetengeneza migogoro wenyewe kwa kumjengea tuhuma zisizo na
ushahidi kama taarifa kutoka makao makuu ya chama kuhusu nyendo za ZZK
toka mwaka 2008 kwa kupokea pesa toka CCM, mbona hamjatuletea ushahidi
wa uhakika nasi tukajihakikishia?
Matokeo yake kila mmoja ameona utofauti wa CHADEMA ya mwaka 2013 na CHADEMA ya mwaka 2014.
Kwenye hili swala la leka dutigite, NSSFna TANAPA mmefanya uchunguzi wa kutosha na mkapata uhakika na mlichopeleka bungeni?
Tunataka ushahidi hapa ili na wananchi tujihakikishie sio mnatuletea propaganda za kijinga hapa na kuanza kuaminisha watu.
Nimesoma ufafanuzi wa Zitto mwenyewe, NSSF na TANAPA nimesikitika sana
kuona kuwa maelezo haya kama ni ya kweli basi CHADEMA ndio itazidi
kupoteza mvuto.
Nashindwa kuwaelewa na hawa washabiki wanaoshinda humu wakishabikia ujinga bila hata kufikiri ilimradi Mbowe kasema.
Watu wanabaki kuchangia changia ujinga wao humu hata katika ujenzi wa
chama hawaonekani wakidhani ndio ukomavu wa chama kumbe ndio wanazidi
kukibomoa chama.
Mnajifanya wanachama wa CHADEMMA kwa kutetea hata ujinga wa baadhi ya
viongozi ndio mnazidi kukimaliza chama, mfano huyu huyu ZZK alipoongelea
kidogo habari za Mbowe wengi wenu mlianza kulalamika kwanini aongelee
habari za Mbowe.
Sasa ZZK sio binadamu kama alivyo Mbowe au kiongozi mwingine anayeweza kuumia anapozushiwa na kuchonganishwa kwa wananchi?
Mashabiki nawashauri acheni kupumbazwa.
0 comments:
Post a Comment