Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeilipua Serikali kwa kushindwa kudhibiti utoroshwaji mkubwa wa fedha kwenda nje.
Msemaji wa kambi hiyo, John Mnyika alisema katika kipindi cha miaka 39
kuanzia 1970 hadi 2008, Sh9.6 trilioni zilitoroshwa kiharamu kwenda nje.
“Utoroshaji wa fedha hizi unasadikiwa kutokana na ukwepaji wa kodi, na
misamaha mikubwa ya kodi,” alisema Mnyika na kuongeza; “Fedha nyingine
zilitokana na usiri mkubwa wa mikataba baina ya wawekezaji na Serikali,
upotoshaji wa bei katika biashara na rushwa katika mikataba na
wawekezaji” alisema.
Mnyika alisema Serikali ya CCM haiwezi kukwepa kuwajibika kwa sababu
utoroshaji wa mapesa yote haya umefanyika wakati na CCM ipo madarakani, ”
alisema.
Mnyika alifafanua, utoroshaji huo wa fedha ulifanyika kwa mafungu na kutolea mfano mwaka 1980, Dola 570. 6 milioni zilitoroshwa.
Fedha hizo zilitoroshwa wakati hayati baba wa Taifa mwalimu Jullius
Nyerere akiwa madarakani na dola 1,566 milioni zikatoroshwa 1985 wakati
wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
“Jambo la kusikitisha zaidi mwaka 2002 zilitoroshwa jumla ya Dola za
Marekani 1,1010 milioni katika kipindi ambacho Rais Benjamin Mkapa yuko
madarakani,” alisema Mnyika.
Mnyika alisema kambi hiyo imesikitishwa na kitendo cha Bunge kushindwa
kuisimamia kikamilifu Serikali hususan Wizara ya Nishati na Madini.
Alisema fedha zote zilizotoroshwa nchini tangu mwaka 1970 mpaka 2008 zinaweza kurejeshwa nchini kwa kuanzia na kuzibaini zilipo.
“Uchunguzi wa kina ufanyike kuzuia fedha hizo katika akaunti za benki
zilipotunzwa nje ya nchi na hatimaye kurejesha fedha hizo nchini,”
alisema.
Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) cha Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) kimetakiwa kukusanya taarifa za kiintelijensia na kuziwasilisha
Takukuru ili uchunguzi ufanyike.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri kutokana na skendo hii iliyoikumba serikali ya utoroshaji wa fedha nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment