Facebook

Saturday, 31 May 2014

Arsene Wenger aongezwa mkataba Arsenal


Arsene Wenger ametia saini mkataba wa miaka miwili kama meneja wa klabu hiyo hadi mwaka 2017.
Wenger, 64, ameongoza Arsenal na kufanikisha ushindi wa mataji 8 tangu kujiunga na klabu hiyo Septemba mwaka 1996.
Msimu huu aliweza kuongoza timu hiyo hadi kufuzu kwa mara ya 17 kwa kombe la klabu bingwa ulaya na kupata ushindi aliosubiri kwa hamu kwa miaka tisa dhidi ya Hull City katika fainali ya kombe la FA Cup.
Wenger alikuwa anafika ukingoni mwa mkataba wake mwaka huu
Arsenal ilikuwa haijawahi kushinda taji la nyumbani tangu mwaka 2005 ingawa walifika fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya mwaka 2006.

Rekodi ya Wenger

Arsen Wenger
  • Ligi ya Premier:1998, 2002, 2004
  • Kombe la FA:1998, 2002, 2003, 2005, 2014
  • Kombe la Community Shield:1998, 1999, 2002, 2004
  • Kombe ya ligi ya klabu bingwa nafasi ya 2: 2006
  • Nafasi ya pili kombe la Uefa Cup:2000
  • Nafasi ya pili Kombe la League:2007, 2011
Wenger, ambaye sasa ni meneja mkongwe zaidi katika ligi ya Ulaya baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu, mwezi Mei mwaka 2013, anasifika kwa kuleta mawazo mapya kuhusu michezo na lishe bora katika soka Uingereza.
''Huyu ndiye mtu anayefanya kazi mwa saa 24 kila siku,'' alisema mlinda lango wa zamani wa Arsenal Bob Wilson.
"anachukia sana kushindwa. Alileta mageuzi makubwa, katika kila sekta ya mchezo huo nchini Uingereza. Watu wanadhani kuwa ana mamlaka sana lakini mtu ambaye anajitolea sana kwa mchezo huu ni mtu anayethaminiwa sana.''
Ushindi mkubwa wa Wenger ulikuwa wakati ambapo alishinda kombe la ligi ya Premier kati ya mwaka 2003-04 alipokuwa na wachezaji kama vile Thierry Henry na Patrick Vieira.
Wenger alimsajili Mesut Ozil kwa kima cha dola milioni 42.4 kwa msimu ambao umekamilika.
Lakini licha ya hali ya suitofahamu kuhusu mustakabali wa Wenger mwezi Januari, mkurugenzi mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alitabiri kuwa Wenger huenda akaongezewa muda Arsenal

0 comments:

Post a Comment