Facebook

Saturday 31 May 2014

Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3


Kampuni kubwa ya teknolojia Apple imethibitisha kwamba itanunua vipokea sauti na huduma ya kusikiliza muziki kupitia kwenye mtandao wa inteneti kutoka kampuni ya Beats Electronics katika makubaliano ya dola bilioni 3.
Hayo yakiwa ni makubaliano makubwa katika historia ya miaka 38 ya kampuni hiyo.
Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza muziki kwenye mtandao.
Pamoja na ununuzi huo, waanzilishi wa Beats Jimmy Lovine na msanii mtajika katika mtindo wa kufoka na Hip Hop Dkt. Dre watajiunga na kampuni hiyo ya kiteknolojia.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook alisema kuwa mkataba huo ungewezesha kampuni hiyo ‘kuendelea kutengeneza bidhaa na huduma za muziki zenye ubunifu duniani.’
Beats ilianzishwa na mzalishaji wa muziki Jimmy Lovine na nyota wa mziki wa kufokafoka, Dr. Dre, na mitambo hiyo imejulikana kuwa bora zaidi hadi siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple ina huduma ya iTunes ambayo ndio kubwa zaidi duniani inayohusiana na mziki, na ilianzisha kituo cha radio cha iTunes mwaka uliopita.

Ijapokuwa kampuni hiyo ya Carlifornia ndio walikuwa waanzilishi wa zamani wa mziki wa mfumo wa dijitali, imekuwa ikikumbwa na ushindani mkubwa kutoka kwenye huduma zinazolipiwa kama vile Spotify, Pandora na Rdio.
Hata hivyo, huduma ya mziki ya Beats ina wateja wapatao 110,000 pekee waliojisajili ikilinganishwa na Spotify ilio na watu milioni 10 waliojisajiliwa.
Mkataba huo na kampuni ya Beats imeonyesha kudidimia kwa Apple ambayo hujulikana kwa kutengeneza bidhaa mpya wala sio kununua kampuni ndogo ndogo kama wanavyofanya wapinzani wao Google.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata stori mbalimbali kama hizi zinazojiri sehemu mbalimbali za dunia.Jukumu letu sisi ni kukuhabarisha.

0 comments:

Post a Comment