Facebook

Saturday, 31 May 2014

Google kufuta historia ya watu Ulaya

Google ina wasiwasi kuwa mataifa kandamizi yatafurahia sana amri ya mahakama Ulaya
Kampuni ya Google inatarajiwa kuzindua huduma ambayo, itawawezesha raia wa Ulaya kuomba viambatanishi vya mitandao yenye taarifa kuhusu maisha yao kufutwa
Google ambao hutumiwa kwa ukubwa duniani kutafuta taarifa imesema kamati ya wakurugenzi wakuu na wataalamu wa kujitegemea wataunda mpango wa muda mrefu kushughulikia maombi hayo ya watu kutoka Ulaya.
Hatua hiyo inajiri baada ya mahakama ya haki Ulaya kuamua kwamba viambatanishi vya data za zamani au zisizo muhimu za watu zinapaswa kufutwa iwapo watu wataomba hivyo.
Mkurugenzi mkuu wa Google, Larry Page amesema kampuni hiyo itafuata hukumu hiyo ya Ulaya lakini ameonya huenda ikaathiri ubunifu na ikafurahisha nchi zenye watawala wakandamizaji.

0 comments:

Post a Comment