ZIMEZAGAA
ripoti huko Ulaya kwamba Meneja mpya wa Manchester United Louis van
Gaal hana nia ya Toni Kroos wa Bayern Munich na Cesc Fabregas na badala
yake anawataka Wachezaji wa Uholanzi ambayo ndie Kocha wa Timu ya Taifa.
Akiwa Kambini pamoja na Timu ya Holland
inayojitayarisha kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza huko
Brazil hapo Juni 12, imedaiwa Louis van Gaal anataka kuwachukua
Wachezaji wawili walioko Kambini humo wanaochezea Klabu ya Feyenoord,
Jordy Clasie and Bruno Martins Indi, ili wajiunge nae Old Trafford mara
baada ya Kombe la Dunia.
Pamoja na hao, pia inasemekana LVG
anamtaka Mchezaji wa AS Roma, Kevin Strootman, licha ya kuwa sasa yupo
muda mrefu nje ya Uwanja akiuguza Goti lake badala ya Kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
Watatu hao, Clasie, Indi na Strootman,
ni Waholanzi wenye sifa kemkem za umahiri mkubwa kiasi ambacho LVG sasa
ameuagiza Uongozi wa Man United uanze mazungumzo Klabu zao na kumaliza
kazi ya Uhamisho wao kimya kimya ili isije ikaonekana kama yeye, ambae
ni Kocha wa Uholanzi, ametia mkono wake.
Indi na Clasie, wote wakiwa na Miaka 22
kila mmoja, wamejipatia sifa kubwa Klabuni kwao Feyenoord kiasi ambacho
Clasie Msimu huu amelazimika kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Holland na pia
Nahodha wa Holland, Robin van Persie, ambae pia ni Mchezaji wa Man
United, kukiri Clasie ni Paul Scholes mpya.
Nae Bruno Martins Indi, Sentahafu Mrefu, mwenye nguvu na akili, ni nguzo imara ya Feyenoord na Holland.
0 comments:
Post a Comment