Facebook

Tuesday, 27 May 2014

Cameroon yashinda licha ya kuwa na majeruhi!!!

Cameroon yashinda ingawa tatizo la majeraha laongezeka.
Nahodha wa Cameroon Samwel Eto’o katika mechi ya kujipima nguvu ambayo The indomitable Lions iliishinda Macedonia mabao 2-0 nchini Austria.
Etoo alipumziswa huku timu hiyo ikiendelea kukumbwa na majeraha zaidi kabla ya kombe la dunia.
Mshambulizi huyo wa Chelsea hakuchezeshwa kutokana na jeraha la goti, huku Cameroon ikimpoteza mshambulizi mwingine Pierre Webo kutokana na jeraha siku ya Jumatatu punde baada ya kufunga.
Jean-Eric Maxim Choupo-Moting baadae akaongeza bao la pili.
Kipa Charles Itandje, mlinzi Jean-Armel Kana-Biyik na viungo Edgar Salli, Jean II Makoun na Stephane Mbia wote wanauguza majeraha tofauti.
Cameroon bado wana mechi za kujipima nguvu dhidi ya Paraguay, Ujerumani na Moldova kabla ya kombe la dunia.

Related Posts:

  • RONALDO, MOURINHO WAPATA TUZO ZA KARNE Mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d'Or Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji wa karne nchini Ureno, katika sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya shirikisho la kandanda la nchi hiyo. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho am… Read More
  • WANYAMA NJE KWA WIKI TANO Kocha wa Southampton, Ronald Koeman ana wasiwasi kuwa huenda Victor Wanyama akakosa kucheza kwa hadi wiki tano baada ya kuumia msuli wa paja katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Ipswich. Wanyama alitolewa muda mfupi kab… Read More
  • Mchezaji mpira wa kike adhaniwa kuwa mwanaume. Kumekuwa na vitendo kadhaa vya kuwatilia mashaka wanamichezo wa kike hasa pale wanapokuwa na uwezo mkubwa kuliko kawaida na mashaka zaidi hutiliwa kwenye uhalisia wa jinsi zao ambapo wengi huhofiwa kuwa si wanaw… Read More
  • BantuTZ MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO JANUARI 17   BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandik… Read More
  • BERAHINO AFUNGIWA KUENDESHA GARI MIEZI 12 Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino amepigwa marufuku kuendesha gari kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kukiri kosa la kuendesha gari akiwa amelewa. Berahino, 21 alikamatwa na polisi saa za alfajiri Oktoba 22 mwaka … Read More

0 comments:

Post a Comment