Facebook

Friday, 30 May 2014

Zitto Kabwe awajibu Chadema aalio Mtuhumu kwa ufisadi Kupitia Leka Dutigite

Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka. 

Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii. Gombe Advisors ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara.

Wasanii wa Kigoma wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo.

Leo mpigie simu mfanyakazi yeyote wa NSSF utasikia kazi ya wasanii hao. Kwa namna yeyote ile hii ni ishara ya kukosa ubinaadam maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote ya kifedha Leo wala kesho kwa LekaDutigite na Gombe Advisors. 

Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama chao, pole ninayopewa ndio hiyo. 

Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.

By Zitto Kabwe

Endelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali zenye ukweli halisi

0 comments:

Post a Comment