Huduma za simu iitwayo Silver
line iliyoanzishwa kusaidia wazee wanaokumbwa na upweke huko Uingereza
imepokea idadi kubwa ya wapigaji simu.
Zaidi ya simu mia elfu zimepokelewa katika kipindi cha miezi sita tangu huduma hiyo kuanzishwa.Nusu wa waliopiga simu wamesema wanaeza kukaa kutwa bila kuzungumza na mtu , ilhali mmoja kati ya kumi wakasema huchukua hata zaidi ya wiki nzima bila kupata mtu wa kuzungumza nao.
Utafiti wa kisaikolojia wasema upweke mwingi unaeza kuleta madhara kama vile majonzi, msongo wa mawazo na athari nyenginezo za kiafya na hasa kiakili.
Tahadhari imetolewa kwa nchi zinazoendelea hasa barani Afrika kufanya jitihada kuzuia mmomonyoko wa kimaadili na utamaduni wa kutunza wazee ili kuepukana na hali kama hiyo.
0 comments:
Post a Comment