Uchina imeanza kulegeza sheria
zake za mpango wa uzazi, na sasa inapiga kampeni yenye lengo la kuongeza
angalau watoto millioni mbili zaidi wanaozaliwa kila mwaka.
Serikali itaongeza wakunga na wahudumu sambamba
na kupanua nafasi hospitalini na kuongezwa idadi ya vitanda na vifaa
nyenginevyo.Lakini mwaka jana serikali iliianza kulegeza kamba kwa kusema iwapo mmoja wa wazazi amekuwa mtoto wa pekee katika familia basi anaweza kuzaa mtoto wa pili.
Japo hatua za awali zilichukuliwa kukabiliana na idadi kubwa ya watu nchi humo, sasa kumetokea mapungufu ambayo yanahitaji kusawazishwa.
Hatua hiyo mpya pia huenda ikaleta afueni kwa wengi kwani sera hiyo ya mtoto mmoja kwa familia ilikabiliwa na changamoto nyingi.
Visa na mateso kwa baadhi ya wazazi na watoto huripotiwa huku watoto vilema, wagonjwa au wa jinsia isiyopendelewa na wazazi wao kubaguliwa na kutelekezwa.
0 comments:
Post a Comment