Facebook

Saturday 31 May 2014

China yakusanya hawa watu Uwanja wa Mpira na kuwahukumu kifo.

 china2 
Watu 55 nchini China wamekumiwa kutumikia adhabu mbalimbali kwa makosa ya ugaidi, uhalifu wa kutumia silaha pamoja na mauaji, hukumu iliyotolewa katika Jimbo la Kaskazini Magharibi la Xinjiang mbele ya umati mkubwa wa watu katika Uwanja wa mpira
Kwa mujibu wa ripoti za shirika la habari la nchi hiyo, Washtakiwa hao ambao walifikishwa mbele ya umati wa takribani watu elfu 7,000 walihukumiwa adhabu mbalimbali huku watatu kati yao wakihukumiwa adhabu ya kifo.

china1
Maafisa wa nchini China wamevishutumu vikundi vya kijeshi vya Uigher ambao ndio sehemu kubwa ya wahalifu hao kwa kusababisha kukua kwa idadi ya mashambulizi katika nchi hiyo.
china3
Picha kutoka katika uwanja huo zimeonyesha magari makubwa ya polisi yakiwa yameegeshwa karibu na kundi kubwa la wahalifu hao kuhakikisha ulinzi wa kutosha huku idadi kubwa ya watu wakishuhudia hukumu hiyo ikitolewa.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kwa wakati muafaka.

0 comments:

Post a Comment