Kampuni kubwa ya utengenezaji wa magari aina ya Ambassador ya nchini
India imefunga huduma zake za uzalishaji kwa madai ya kugubikwa na
madeni na kukosekana na mahitaji ya ya gari hilo ambalo liliuzwa sana na
kuweka matabaka katika nchi hiyo kutokana na gharama zake.
Kiwanda hicho cha Hindustan ambacho ni cha zamani zaidi kuliko vyote
nchini humo imefunga huduma zake katika Jimbo la Uttarpara Magharibi mwa
Bengal ambako imekuwa ikitengeneza magari ya aina hiyo tangu mwaka
1957.
Afisa mkuu wa kiwanda hicho amesema kuwa kazi katika katika kiwanda
hicho zimesitishwa na wamefanya hivyo kuhakikisha kiwanda hicho
hakitumii fedha zaidi na kuwafanya kuweka mipango mipya ya kukirudisha.
0 comments:
Post a Comment