Bingwa mtetezi wa michuano ya French Open Serena Williams ametolewa katika michuano hiyo na Gabine Muguruza kutoka Spain katika siku ya nne.
Mapema dada yake Serena, Venus, alitolewa na Anna Schmiedlova kutoka
Slovakia. Hii ni mara ya kwanza kwa
Serena kushindwa kuingia katika wiki ya pili ya michuano mikubwa kama
mchezaji wa juu.
Matumaini ya dada hawa wawili kukutana katika raundi ya
tatu sasa hayapo, na itakuwa kati ya Muguruza na Schmiedlova.
Endelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali za burudani na michezo kwa wakati na muda muafaka.
0 comments:
Post a Comment