Facebook

Thursday, 29 May 2014

Mgomo wayumbisha Uchumi Afrika Kusini


Vyama vya wafanyikazi Afrika kusini vinaungwa mkono na wengi hivyo migomo yao huwa mikali.
Mazungumzo yaliyonuiwa kumaliza mgomo katika sekta ya madini Afrika kusini yamesambaratika.
Waziri wa maswala ya madini nchi humo ,Ngoako Ramatlhodi, amesema juhudi zote za kupatanisha wenye makampuni ya migodi na chama cha wafanyi kazi cha AMCU wamegonga mwamba.
Mahakama ya kazi pia inaonekana kushindwa katika juhudi za punde zaidi kumaliza mgomo ulioendelea kwa miezi minne. Mgomo huo unmetishia kupormosha sekta ya madini hasa uchimbaji wa madini ya platinum nchin Afrika Kusini.
Bw. Ramatlhodi sasa ameonya kuwa mgomo huo unaupelekeka Uchumi wa Afrijka kusini pabaya,huku sekta ya viwanda na uuzaji nje wa bidhaa za Afrika kusini nazo zikiripotiwa kufifia..
Familia za wachimba migodi pia zimeathirika pakubwa.
Mara nyingi migomo ya wafanyikazi hukumbwa na ghasia zinazosababisha vifo na majeruhi.
Wachimba migodi zaidi ya elfu sabini wa Platinum wanadai malipo bora na kuboreshwa mazingira ya kufanya kazi.
Hata hivyo kuna wachache ambao wanataka kurudi kazini, lakini wanahofia maisha yao na wenzao wanaoendelea na mgomo huku kukiripotiwa visa vya mashambulio, na wachimba migodi watano kuuawa katika wiki mbili zilizopita.
Baadhi ya waekezaji wameilaumu serikali ya rais Jacob Zuma kutochukua msimamo thabiti juu ya suala hili.

0 comments:

Post a Comment