Facebook

Saturday 31 May 2014

Unakijua wanachokifanya makondakta nchini Thailand wanapohitaji kujisaidia wakati wa foleni ndefu.

bus_1
Tatizo la kukithiri kwa msongamano wa magari na kukaa kwa muda mrefu kwenye foleni kwa siku nzima, Makondakta wa mabasi nchini Thailand wametafuta suluhisho binafsi pale wanapohitaji kujisaidia wakiwa barabarani kwa kuvaa nepi za watu wazima.
Kutokana na kukithiri kwa msongamano barabarani, makondakta hao wa mabasi makubwa katika mji mkuu wa Bangkok wanatumia muda mrefu barabarani kwenye foleni hali inayowafanya kubanwa haja na kuwalazimu kusubiri hadi kwenye vituo kwenda kujisaidia katika vyoo vya pembezoni.
bus2
Mmoja wa wafanyakazi hao amesema wamekuwa wakipata matatizo katika njia za mkojo kutokana na kukaa na haja kwa muda mrefu hivyo huwalazimu kuvaa nepi za watu wazima wanazobadilisha mara mbili kwa siku wanapofika kwenye vituo vikubwa vya mabasi.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua stor mbalimbali zinazotokea pande zote za dunia kwa wakati na muda muafaka

0 comments:

Post a Comment