Wasichana wawili wa kihindi
waliopatikana wakiwa wananing'inia kwenye mti katika jimbo la Uttar
Pradesh, walikuwa wamebakwa kisha wakanyongwa.
Polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja amekamatwa
kuhusiana na mauaji hayo huku polisi watatu wakiachishwa kazi kwa
kutosajili kesi hiyo iliporipotiwa kuwa wasichana hao walikuwa
wametoweka, kabla ya kupatikana wakiwa wameuawa.Ubaguzi dhidi ya wanawake umekita mizizi katika jamii nyingi nchini India.
Visa vya dhuluma za kingono vimeendelea kukithiri nchini India tangu mwaka 2012 ambapo msichana mmoja alibakwa na genge la vijana hadi kufa
Serikali ililazimika kuweka sheria kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutenda vitendo vya dhuluma za kingono baada ya maandamano kufanyika kote nchini kufuatia shambulizi hilo.
Polisi mmoja alisema kuwa wasichana hao walikuwa na uhusiano wa kifamilia na walipatwa wakiwa wananing'inia kwenye mti kijiji cha Badaun mnamo siku ya Jumatano.
Alisema kuwa polisi wanawasaka wanmaume wawili waliowabaka wasichana hao na kisha kuwanyonga.
Wasichana hao walichomwa kuambatana na tamaduni za maziko ya kihindi Jumatano.
Polisi wanasema wanachunguza ambavyo wasichana hao walipotea, kubakwa na kisha kuwekwa kwenye mti.
0 comments:
Post a Comment