Yerusalemu, Israel. Malumbano makali ya maneno na hoja
yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis na Waziri
Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu lugha gani aliyotumia Yesu Krtisto
miaka 2,000 iliyopita.
Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya siku tatu ya
Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni ziara yake ya kwanza
tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika ardhi ya nchi hii.
Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati akimweleza Papa Francis kwenye
mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.
Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya
mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo.
Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu
alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”
“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua
Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.
Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia tofauti na watu
wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya Papa Francis katika
nchi takatifu.
Mtaalamu wa masuala ya lugha, raia wa Israel, Profesa
Ghil’ad Zuckermann ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba wawili hao,
Netanyahu, ambaye ni mtoto wa mtaalamu wa historia ya Kiyahudi na Papa Francis,
kiongozi wa kiroho anayeongoza waumini bilioni 1.2 Wakatoliki, kila mmoja ana
hoja. “Yesu alikuwa mzungumzaji wa Kiaramaiki,” anasema Profesa Zuckerman
kuhusu lugha hiyo ambayo imetoweka yenye uhusiano na Kiebrania. “Pia, anaweza
kuwa alizungumza na kufahamu Kiebrania, lugha ambayo ilitumika kwenye
maandiko.”
Prof Zuckermann alisema kuwa wakati wa Yesu, Kiebrania
kilizungumzwa na watu wa madaraja ya chini - “ambao ndiyo aliowahubiria”.
Mojawapo ya vitu vingi katika eneo la Mashariki ya Kati hadi sasa ni kuhusu
utata wa Yesu, utata huo umechukua pia sura na mtazamo wa kisiasa.
Yesu, Myahudi alizaliwa kwenye mji wa Bethlehemu ambao
ulikuwa chini ya himaya ya Warumi, kwenye Mkoa wa Yudea, katika ardhi
inayoshikiliwa kwa sasa na Israel kwenye Ukanda wa Magharibi.
Alikulia mjini Nazareth , akaendesha utume kwenye mji
mwingine wa Galilea, ambao pia uko kaskazini mwa Israel, alifia mjini
Yerusalemu, mji ambao unatukuzwa na Wayahudi, Wakristo na Waislamu, ambao
unagombewa na tawala za Israel na Palestina hadi sasa.
Kwa upande wao, Wapalestina wamekuwa wakidai kuwa Yesu ni
Mpalestina. Hata hivyo, utawala wa Israel umekuwa ukipingana na mtazamo huo.
0 comments:
Post a Comment