Facebook

Saturday, 31 May 2014

Matamshi kuhusu ubakaji yakera India


Matamshi ya mwanasiasa mmoja mwanamke nchini India kuhusu ubakaji yamelaaniwa na watu wengi kote nchini humo.
Asha Mirge, ambaye ni mwanachama wa kikundi cha viongozi wanawake serikalini katika jimbo la Maharastra, amesema kuwa wanawake pia wanachangia pakubwa kwa wao wenyewe kubakwa kutokana na mavazi pamoja na wanavyotembea na hata kuzungumza.
Amehoji kwa nini wanawake hutoka nje nyakati za usiku.
Matamshi haya yaliyozua gumzo katika vyombo vya habari kote nchini India, yamesababisha kero kubwa kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wanasiasa wengine.
Bi Mirge hata hivyo ameomba radhi kwa matamshi yake akisema yametiwa chumvi.
Inda imekuwa ikimbwa na visa vya mara kwa mara vya ubakaji kiasi cha serikali kubuni sharia kali dhidi ya wabakaji.
Ni wiki jana tu ambapo wazee wa kijiji waliamrisha kubakwa kwa mwanamke ambaye alikuwa na uhusianao wa kimapenzi na mwanamume ambaye sio wa kutoka jamii moja naye.

0 comments:

Post a Comment