Facebook

Thursday, 29 May 2014

Man Utd wapanda dau kwa Miranda..Crystal Palace yatema 12

MIRANDA






















WAKATI zimeibuka taarifa thabiti huko Spain kwamba Manchester United wako njiani kumsaini Beki hodari wa Atletico Madrid, Miranda, Klabu ya Ligi Kuu England, Crystal Palace, imewatema Wachezaji wake 12 kwa ajili ya Msimu mpya.

MIRANDA KWENDA MAN UNITED!
KUONDOKA kwa Mabeki Rio Ferdinand na Nemanja Vidic kumeifanya Man United kuhaha kusaka Mabeki kuziba nafasi hizo na habari kutoka Jarida maarufu huko Spain, AS, zimethibitisha kuwa Mabingwa hao wa zamani wa England wako mbioni kulipa Pauni Milioni 24 ili kumchukua Miranda, Beki kutoka Brazil mwenye Miaka 29, na ambae ndio nguzo imara iliyoifanya Atletico Madrid kutwaa Ubingwa wa La Liga Msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza toka 1996 na kuwafikisha Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI waliyofungwa 4-1 na Real Madrid.
AS limedai kuwa Miranda, ambae ameichezea Brazil mara 3, hivi sasa yupo kwenye hekaheka ya kutafuta Shule huko Jijini Manchester kwa ajili ya Watoto wake.
Miranda alijiunga na Atletico Mwaka 2011 akitokea Sao Paulo ya Brazil na tangu wakati huo kila Msimu Atletico imetwaa Kombe walipotwaa EUROPA LIGI Mwaka 2012, Copa del Rey Mwaka 2013 na La Liga 2014.
AS imedai Atletico watambadili Miranda kwa kumnunua Beki wa FC Porto ya Ureno, Eliaquim Mangala ambae pia anawindwa na Chelsea na Manchester City.
PALACE YATUPA NJE 12!!
Crystal Palace imewatema Wachezaji 12 baada kusafisha Kikosi chao kwa ajili ya Msimu mpya.
Mabeki Dean Moxey, Danny Gabbidon na Jonathan Parr, Straika Aaron Wilbraham na Kipa Neil Alexander hawatapewa Mikataba mipya.
Wengine walioachwa ni Chipukizi Osman Sow, Ibra Sekajja, Quade Taylor, Derek Tieku, Ross Fitzsimons, Tom King na Alistair Gordon.
Hata hivyo, Crystal Palace inataka kuwabakisha Kipa Julian Speroni, Marouane Chamakh na Kagisho Dikgacoi licha ya Wachezaji hao Mikataba yao kumalizika na sasa yapo mazungumzo kati ya pande hizo.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na usajili

0 comments:

Post a Comment