Facebook

Saturday, 31 May 2014

Real Madrid yaadhibiwa kwa ubaguzi wa rangi

Mabingwa wa Champions League shurti kutangaza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi-UEFA
Shirika la kandanda la Europa, UEFA, limeiwekea vikwazo timu ya mpira ya Real Madrid kwa makosa ya mashabiki wao, waliotoa ishara na kejeli za ubaguzi wa rangi wakati wa moja ya mechi zake.
Je ni sawa Real Madrid kuadhibiwa na UEFA kwa sababu ya makosa yaliyofanywa na mashabiki wake?
Tukio hilo lilifanyika April wakati wa mechi ya nusu fainali kati ya mabingwa hao wa sasa wa kombe hilo la UEFA, na mahasimu wao,mabingwa wa zamani wa Bayern Munich.
Miongoni na adhabu walizopewa ni kufunga maeneo mawili ya uwanja wao wa Bernabeu wakati wa mechi yao itakayokuja ya UEFA na watapaswa kuweka mabango yaliyo na maandishi 'No to Racism' yaani 'Twakataa ubaguzi wa rangi!.

0 comments:

Post a Comment