Facebook

Tuesday 27 May 2014

Rick Ross Na Tattoo Nyingine Usoni, Ni Ya Jina La Mixtape Yake.

 rickross-NikkoHurtado
Rick Ross amechorwa jina la moja ya Mixtape zake kwenye uso wake hivi kaibuni na mchoraji maarufu Nikko Hurtado.Tattoo hii ya  “Rich Forever” ipo kwenye kidevu cha rapper huyu chini tu ya mdomo wake.
Picha za tattoo hii zimesambazwa na mchoraji Nikko Hurtado aliyewahi kumchora rapper Game picha ya Nelson Mandela December 2013 .
“Rich Forever” ni jina la mixtape ya Rick ross iliyotoka 2012 na kumpa heshima kubwa kwenye rap kani ilikuwa mixtape ya kiwango cha juu na ilitoa nyimbo zilizoshika chati.
Rozay alihojiwa kuhusu Kauli ya Rich Forever mwaka 2012 nakusema ” Maana yake ni kuwa tajiri wa mawazo, ubunifu na mbinu zaidi, huo ni utajiri wa milele”. Ilikuwa interview ya  Mixtape Daily.
Hii ni miongoni mwakazi alizowahi kufanya mchoraji huyu, Hii alichorwa rapper The Game aka Game.
 gg

0 comments:

Post a Comment