Facebook

Thursday, 29 May 2014

Moto waua wagonjwa 21 hospitalini Korea

Wazima moto wakiwasili hospitalini kukabiliana na moto Korea Kusini.
Moto Uliozuka Hospitalini wauwa watu 21 Nchini Korea Kusini.
Wagonjwa wapatao 20 pamoja muuguzi wameuawawa baada ya moto mkubwa kuwaka hospitalini katika jimbo la Janseong nchini Korea Kusini, huku wengine 6 wakiwa hali mahututi baada ya moto huo katika hospitali ya Hyosarang iliyoko kilomita 300 kusini mwa Seoul.
Wengi wa walioaga dunia wanafikiriwa kuwa wazee wenye umri wa kati ya miaka 70 na 80 na wasioweza kutembea.
Maafisa walisema kuwa wengi waliokufa walikosa hewa kutokana na gesi zenye sumu.

Moto huo ulizimwa kwa takribani nusu saa.
Moto huo ulianza muda mfupi tu baada ya saa sita usiku katika hilo jumba lenye orofa tatu.

Vyombo vya habari vinaarifu kuwa wengi wa wagonjwa waliokuwa katika orofa ya juu ya jumba hilo walishindwa kujiokoa kwa sababu vyuba vyao vilikuwa vimejaa moshi uliotokana na moto huo.
Muuguzi huyo aliyekufa alikuwa akijaribu kuzima moto kwa kutumia kizima moto kulingana na shirika la Agence-France Presse.
Ripoti ya shirika la Yonhap ilisema kuwa polisi walisema kuwa jumba hilo lilikuwa limefanyiwa uchunguzi wa kiusalama majuzi.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Lee Hyung Seok aliomba msamaha na kuwaambia wanahabari kuwa alikuwa ametenda dhambi kubwa, na kuwa hangetoa visababu wakati watu wameaga dunia.
Tukio hili limekuja wakati wananchi wa Korea kusini wakiendelea kuomboleza vifo vya zaidi ya watu 300 waliofariki katika ajali ya feri iliyotokea mwezi uliopita.
Rais wa taifa hilo Park Geung-Hye ameliomba taifa radhi kirasmi kwa ajali hiyo ya feri, huku akiahidi kuimarisha viwango vya usalama.
Waziri mkuu Chung Hong-won wakati huo alijiuzulu kwa madai ya jinsi serikali ilivyokuwa ikikabiliana na majanga.
Ajali hiyo ya hospitali pia imetokea siku moja tu baada ya watu 7 kuuwawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mkasa wa moto uliozuka katika kituo cha mabasi jijini Goyang.

Related Posts:

  • Magaidi wajifaidisha na uwindaji haramu moja wa Ndovu waliouawa na wawindaji haramu nchini Kenya Makundi ya kigaidi na wanamgambo wamekuwa wakifaidi kutokana na uwindaji haramu wenye thamani ya dola bilioni 213 kila mwaka, na kutishia usalama wa kimataifa… Read More
  • Mkereketwa apigwa risasi na kuuawa Libya Mzee akisaidiwa kupiga kura nchini Libya katika uchaguzi uliodhaniwa ungeimarisha usalama. Wakili mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu nchini Libya ameuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulika… Read More
  • Gavana akabiliwa na kesi ya mauaji Kenya Timamy alikamatwa Jumatano na kufikishwa mahakamani Alhamisi Gavana wa kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mauaji ya zaidi ya watu sitini katika eneo la mpeketoni. Issa Timamy hata… Read More
  • Kenyatta aongoza kwa umaarufu utumiaji wa Twitter Afrika Rais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika. Kenyatta amempiku Rais wa Rwan… Read More
  • Obama aomba pesa awasaidie waasi Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi w… Read More

0 comments:

Post a Comment