Facebook

Friday, 30 May 2014

Umeisikia hii kutoka Skype itakuwa ni shidah

Screen Shot 2014-05-29 at 8.59.32 AM 

Mtandao wa skype ambao umekua ukitumika na watu mbalimbali duniani kama njia ya kuwasiliana huku kila mmoja akipata nafasi ya kumuona mwenzake wa upande wa pili kwa njia ya video, umepata kitu kingine kipya kitachorahisisha mawasiliano zaidi. (Skype Translator)
Unaambiwa kabla mwaka 2014 haujaisha, Microsoft wana mpango wa kuileta hii huduma itumike na kila mtu, yani ni application ambayo inaweza kutafsiri lugha mbalimbali na kuwawezesha watu wanaowasiliana kwa lugha tofauti kusikilizana papo kwa papo mfano mtu anaeongea Kijerumani akaongea lugha hiyo lakini wa upande wa pili akawa anamsikia kwa Kiingereza.
Wanasema hii imekuja kuvunja mipaka ya matumizi ya lugha, sasa itakuwezesha kuwasiliana na kuelewana na yeyote ulimwenguni kwa sababu inayachukua uliyozungumza na kuyaweka kwenye lugha uliyochagua, sauti inakua ileile ya kiume kama wewe ni Mwanaume au ya kike kama wewe ni Mwanamke.
Kitu kimoja ambacho sijakifahamu ni kama Kiswahili kitafanya kazi ndani yake

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya sayansi na teknolojia

Related Posts:

  • MAAJABU:Upandikishaji wa kichwa sasa unawezekana Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa. Madaktari watazindua mradi huo katika k… Read More
  • Yahoo kufungua ofisi zao ChinaKampuni ya mtandao YAHOO inatarajiwa kufunga afisi yake ya mwisho katika eneo la China bara. Kampuni hiyo kama kampuni nyengine za kiteknologia imekuwa ikikabiliwa na ushindani mkubwa nchini Uchina kutoka kampuni nyengine za … Read More
  • Ndege inayotumia mwanga wa jua yafanyiwa majaribio Jaribio la kuruka angani kwa ndege inayotumia umeme wa jua limeanza. Ndege hiyo iliruka kutoka Abu Dhabi,kabla ya kutua Oman na kuelekea nchini India.Ziara yake katika sayari inatarajiwa kuchukua miezi mitano ikiwa na changam… Read More
  • Facebook kufungua huduma mpya kama "WhatsApp" Mtandao wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya messenger kwa wajenzi. Habari hizo zilitangazwa na Mark Zuckerberg katika kongamano la nane la wajenzi lililofanyika mjini San Fransisco. Zaidi ya programmu 40… Read More
  • Kampuni ya Smartwatch kuzindua saa mpyaKampuni ya saa za Smartwatch,Peeble imechangisha zaidi ya dola millioni 10 kwa ajili ya programu yake mpya ya wakati katika mtandao unaofadhiliwa na makundi ya watu Kickstarter. Mradi huo wa kampuni ya Peebles ni miongoni mw… Read More

0 comments:

Post a Comment