Jana usiku habari zilizoshtua watu wengi ni kuhusu kifo cha director mashuhuri George Tyson. Hivi sasa kuna taarifa ambazo hazijawahi kutolewa na hawa wahusika kuhusu marehemu Tyson.
Zipo tano hadi sasa na zinatoka kwa watu mashuhuri kwenye kiwanda cha burudani.
Jokate Mwegelo amesema kuhusu kazi nzuri aliyokuwa anafanya George Tyson kama director wa The One show ambayo inaruka kupitia TV1
Venessa Mdee hajawai kusema sababu ya kuacha kufanya The One show ambayo alianza hadi ku-shoot. Hivi sasa amesema sababu hiyo akimhusisha George Tyson kama mtu aliyempa moyo kwenye maamuzi yake.
Hemed PHD na yeye anasema kwamba George Tyson ndiye mtu ambaye aligundua kipaji chake cha kuigiza wakati akiwa kwenye Tusker Project Fame.
Kazi kubwa ya George Tyson ilikuwa ni ku-direct vipindi vya TV kama unavyoona hapo chini na juu ambapo AY anamzungumzia baada ya kufanya show ya Boys Boys. Pia Mboni Masimba anamtaja kama director wa show yake.
0 comments:
Post a Comment